Ni kitu gani ulikifanya kwa kutumia nguvu nyingi, muda mrefu au kuomba msaada usaidiwe kabla hujagundua mbinu rahisi ya kukifanya kwa wepesi

Ni kitu gani ulikifanya kwa kutumia nguvu nyingi, muda mrefu au kuomba msaada usaidiwe kabla hujagundua mbinu rahisi ya kukifanya kwa wepesi

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwa muda mrefu sana nimekuwa naweza kunyoosha mashati na makoti lakini linapokuja suala la kunyoosha suruali za vitambaa na kadeti ilinitesa sana kwakweli, nilikuwa naotea otea tu mpaka kuna muda narudia mara tatu kunyoosha suruali moja.

Yaani kulinganisha tu upanga wa suruali ilikuwa mtihani nikinyoosha suruali upanga unakuwa upo nje ya kawaida na sometimes suruali inakuwa na upanga zaidi ya moja.... Hali hii ilinipelekea nipende zaidi jeans.

Kuna siku nacheki youtube ndio nikaona mbinu nyepesi ni kufananisha kila pande chini ya suruali, kwa sasa navaa sana suruali maana shida imeondoka...

Wewe ulifanya kitu gani kwa muda mrefu, nguvu nyingi ama hata kushindwa kabisa lakini sasa unaweza kukifanya haraka kwa ukamilifu ?
 
Kutongoza kwa muda mrefu sasa hivi nikumwaga noti siongei.....
 
Bando langu la wewk la Halotel nilikuwa natumiaga ndani ya siku mbili tu, ila siku hizi bando langu la week natumia week
 
Back
Top Bottom