Ni kitu gani uliwahi fanya ukiwa peke yako.

Shadrack K. Lwila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2016
Posts
4,925
Reaction score
14,287
Wakuu mambo vipi,

Natumai mkopoa sana tu,hivi ni kitu gani uliwahi kukifanya ukiwa peke yako na ukabaki unacheka mwenyewe au ukabaki umestaajabu mwenyewe.

Binasfi niliwahi kunywa maziwa ambayo yalikwisha ingia inzi nilikuja kugundua wakati nimeshameza nzi kadhaa hila nikajipa moyo sababu hakuna aliyeniona.

Kuna siku niliwahi kuanguka chooni nikabaki najicheka mwenyewe nikajisemea moyo labda majini yamenicheka sana.
 
1.Kunusa baadhi ya maeneo ya mwili wako kuona kama yanatoa harufu!, mara nyingine unajikuna kisha unapeleka mkono puani kuona ni harufu gani utaskia.

2. Kuigiza kama unafanyiwa interview. Unajiuliza maswali kadhaa na kujijibu kwa kujiamin huku unatabasamu kana kwamba kuna mtu anakuona.

3. Kutoa uchafu puani kwa kutumia kidole kwa dakika kadhaa, na mtu akitokea ghafla, unajidai unakuna shavu!

4.Kula haraka haraka kwa kificho (tunda, kitafunwa nk) ofisini, nyuma ya mlango nk na kujifuta mdomo ili asigundue mtu!

5. Kutengeneza Sura mbalimbali mbele ya kioo na kuangalia unaonekanaje!

6 Kutoa Hewa chafu kwa sauti (Farting Loud). Hii hairuhusiwi kwenye jamii yetu!

7.Kutoa Haja ndogo wakati wa kuoga

8 Kufanya baadhi ya vitu kwa kutumia miguu badala ya mikono! Kufunga mlango au Kuokota vitu kwa kutumia vidole vya mguuni

9. Kula paketi nzima ya chakula Fulani ambayo pengine ungekula kwa siku kadhaa taratibu
 
10. Umewasahau CHAPUTA members
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]

Dah mkuu lipi unapenda zaid apo?
 
Mimi kuna siku nilikuwa ktk kambi moja nikiwa Kama msaidizi wa kazi kambini, sasa wakati nimepewa mavazi rasmi ya kazi, ilibidi nikayafue kwanza, nikiwa nimeyaloweka sasa naanza kufua na nishafua shati sasa ndio naanza kufua suruani nikasema ngoja nisachi, kusachi nikakuta grenade ktk mfuko wa ile suruali, nilicheka sana, sababu iliyonifanya nicheke ilikuwa kuchanganyikiwa kuliko pitiliza.

Kuna siku tulikuwa tunavuta na mabosi zangu hukohuko kambini, ilikuwa mida ya saa kumi na mbili za jioni tunavuta huku kila mmoja akihadithia mambo mbalimbali ktk nchi aliyotokea, huku Mimi nikitoa kitu cha ugali wa mihogo, jamaa walikuwa wanapenda sana, sasa Nguni ilipokuwa tayari wote tukanawa na kuanzia kula, Ila kuna mwenzetu mmoja ambaye yeye alikuwa m south, akasema kashiba tukala tu kamaliza, ajabu msosi umeisha ye ndo anastuka anaulizia vipi chakula bado? Nilicheka sana..jamaa alisizi na mi.....

Wakati narudi home kwa mbaali namuona mtu akiyumba barabarani huku akinyeshewa na mvua..ghafla namuona karuka sehemu nzuri karukia ndani ya mtaro alafu kafikia kidevu maji yakaanza kupeleka, nikamuopoa, na kum peleka hospital nikamuacha huko. Kesho yake kwenda kumuona nami uliza vipi ndugu ananiambia alivamiwa na majambazi..nilicheka mno
 
Kuna mbongo alipata kazi ya weekend kwenye Gordown ya wine ughaibuni. Siku moja wamemkuta amelala hajitambui kuita ambulance hospital amekuwa na 3 times alcohol over limit kwenye damu. Alipopata nafuu alikutana na P45
 
Kuna mbongo alipata kazi ya weekend kwenye Gordown ya wine ughaibuni. Siku moja wamemkuta amelala hajitambui kuita ambulance hospital amekuwa na 3 times alcohol over limit kwenye damu. Alipopata nafuu alikutana na P45
P45 NI NIN
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
kukata mauno hasa nyimbo za boringo, kama huu mpya wa kofi tshotsho na nyataquance silali bila kukata mauno peke yangu
 
Ngoja nikumbuke!!
Daaah vipo vingi sana.
 
Hahahaha umeuaa [emoji23][emoji23][emoji23]

Wanasema yale unafanya ukiwa peke yako ndo tabia yako/zako....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…