Ni kitu gani...?!


May be,

Stringent vetting kwenye ndoa inaweza kuwa imekaa kinadharia zaidi!! Naamini kuna watu wamefanya vetting ya nguvu na kwa gharama kubwa sana lakini wameishia kusambaratika kabla ya first anniversary!!

Hadi sasa sina hakika ni variables gani ambazo kwa kiasi kikubwa (strongly and reliably) zinaweza kutabiri (predict) mstakabali wa ndoa!!

Na umri huu, bado niko tayari kupigwa shule!!

Babu DC!
 

Babu (naona umetoa ruhusa rasmi) DC hiyo misemo ya Kloro siikatai na inawezekana sana ikawa na kweli ndani yake!

Wa kwanza ntapingana nao kwa kiasi kikubwa kwasababu mara nyingi sio lazima mtu binafsi aexperience kitu fulani kujua kwamba ni kizuri au la!Kitendo cha mimi kua uraiani hakuninyimi mimi uelewa wa nini kinaendelea ndani ya gereza...hakuninyimi mimi imagination na wala hakuninyimi mimi ufahamu wa kutofautisha/kuzifahamu adha za kua gerezani na raha ya kua uraiani!!!Kwa kutumia tu akili/fikra nilizojaliwa naweza kutofautisha jela na uraiani pia faida na hasara za pande zote mbili.Sadly to say...kwangu mimi gerezani hakuna faida yoyote kwangu..na kuwa upande huo wa maisha kutaniondolea furaha yangu kwa kiasi kikubwa sana!!Hivyo basi nitafanya kila niwezalo kuhakikisha siishi jela (japo naweza kuingia kwa bahati mbaya)...kwasababu tayari najua sio sehemu nnayotaka kuwepo.Yani huo ni uchaguzi wangu...na nguvu zangu nazielekeza kwenye kukataa kubadili uchaguzi wangu iwe kwa lazima au hiari!!!

Msemo wa pili umejaa ukweli mwingi!Ila kwangu sijamtukana mama ntilie popote...nilichosema tu ni kwamba SIPENDI kula kwa mama ntilie na uwezo wa kutokula kwa mama ntilie nnao hivyo sitokaa nikubali kula kwa mama ntilie!!

Its all in the mind...kam hutaki hutaki tu!!Kwahiyo ikitokea najua jinsi ya kujiengua... simnyanyasi mtu ili na mimi nisinyanyasike! Pia siamini kwamba naishi ili niwe nalia na kuugulia maumivu kila siku.
 
Ndugu yangu DC haijakaa kinadharia..hapa ndipo ulipo ukweli..tabia siyo fedha mtu hawezi ficha na ktk hili wengi wamelia, hivyo jamii inayomzunguka huyo mchumba ina a-z ya tabia yake na wala haihitaji gharama kufuatilia..taabu vijana wa leo hawaulizi /hawashirikishi watu wazima ktk hili..ndo tunasikia aah huyo alikuwaga shoga toka chuo nk.,tabia ndiyo kitu kinachoweza tabiri hatima ya ndoa babu dc..ndipo waswahili hunena tulijua tu au fupa lililomshinda fisi...au gume gume lililomshinda ..... angaliweza? ni misemo ya kiswazi yenye kusaza ukweliii..babu dc kuchunguza hakujapoteza maana bado..unaweza beba shipa(dume-shoga au mke mchawi) ukajuuuta kuzaliwa..
 

Bibi Lizzy, haya yote ni ya kusadikika....! Maana katika kila ndoa lazima baadhi ya hayo yatokee...! Cha msingi ni kufahamu yafuatayo;
  1. Mara zote mwanamke humkubali mwanaume, pamoja na mapungufu kwa matumaini kwamba huyo mwanaume atabadilika....! Lakini wanaume hawabadiliki....!
  2. Mara zote mwanaume humtokea mwanamke bila kumjua vema, na hivyo anakuwa na imani kuwa huyo mwanamke hatobadilika....! But, normally they do change....!
  3. Hakuna kosa kama kumsamehe binadamu kosa mlilokubaliana kwamba ni kosa kabla ya kosa hilo kufanyika....!
  4. Bora kuishi peke yako, kuliko kupenda bila kupendwa....!
 
Kipenzi chao umelongaa..ila tahadhari, ni kukosea/kubahatisha kuamini tabia ya mtu itabadilika mbele ya safari (amemshindwa mamaye, iweje weye?) unless there is spiritual efforts... kusugua magoti saana..na hata wengine huishia kwa witch drs..dawa ni umakini ktk selection, ILA MUNGU NI MBELE YA YOTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…