KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Maisha yetu hupitia mengi ya maana na vituko ndani yake,tunaweza kushea vituko vya ugomvi tulivyopitia huko tulipotoka.. Binafsi mara ya mwisho kupigana ni enzi za ukindakinda huko japo si mtu wa ugomvi lakini inapobidi lazima Ni ukunje tupambane,bila kusahau pia kwenye mbio nipo vyema..😂
Nakumbuka darasa la tatu nilivamia mchezo usionihusu!,nilikuta mzozo kama Kuna hujuma imefanyika so mi nikaingia nauliza kiubabe lkn nilikuwa natania! Na aliekuwa akicheza alikuwa ni rafiki yangu so alipooana nimekuja kiubabe akaona huyu ndo mtetezi!!! Asalalee sijakaa vizuri yule aliekuwa anacheza huo mchezo ambae alikuwa ni mpinzani wa rafiki yangu nikaona anavua kibegi chake na shati tena huku akisapotiwa na rafiki zake!.. Sasa kijamaa kilikuwa kinaringia kifua kilikuwa kimejazia sijui kilikuwa kinafanyishwa mazoezi na Kaka zake..😅
Mara tukaachiwa uwanja,marafiki zangu wakataka nami nivue shati nikagoma nikawapa begi tu.. tukaupanga so wakati tumeupanga mi huku nishaharibikiwa kisaikolojia maana kijamaa walikuwa wanakisifu kina kifua na tumsuli so mpk tunaupanga ushindi ulikuwa umeelemea kwake!.. hapo komamanga mapigo ya moyo yanapiga kwa spidi isiyofahamika..!
Sasa kile kijamaa kilivyokishenzi sasa pamoja na yote hayo kiliyonayo kikaona hayatoshi wakati anakuja kunishambulia aliaanza kupiga mikelele kana kwamba anakuja kumaliza duh!.. ni kama vile muvi star sasa ndo anakuja kuuwa jambazi muvi iishe wakati ndo tunaanza!.. aisee zile kelele za kijamaa zilinifanya niogope zaidi mi nikaona haya yote yanini..? Kabla hajanifikia nikageuka nikala mbio za maana..😂
Aisee nilichekwa vibaya lkn kugeuka nyuma kijamaa kipo na bado kinapiga kelele huku kikinifata!.. baada ya mbio kadhaa kikaacha nilikuwa nimekizidi mbio kikasimama nami nikasimama so baada ya hapo hasira zikanishika Sasa nikakarudia bila kuangalia ubaunsa wala nini!.. nilikitwikwa mingumi mchezo ukaenda vyema walionicheka wakabadili gia,marafiki zangu nikawapa matumaini wakaanza kunishangilia.. nilipiga kile kibaunsa uchuro mpk kikalia..😂
Japo kilinikwangua na mikucha yake lkn hakikufua dafu..
Nashukuru niliivunja aibu na sifa zilitapakaa darasa kwangu mpk na madarasa mengine nikapata na mpambano mwengine!.. huo sitaki simulia maana nilikabwa kabali inaitwa "USIEMPENDA KAJA!!"😂😂 Ningekufa kama nisingesaidiwa kutoka pale vimtu vyengine kama vichawi tu..😂😂
Karibuni tushee kwa pamoja walau tucheke tuongeze siku za kuishi..