Ni kituo au king'amuzi gani nchini kitaonyesha michuano ya AFCON 2019?.

Ni kituo au king'amuzi gani nchini kitaonyesha michuano ya AFCON 2019?.

Kamtwanje H

Member
Joined
Oct 16, 2010
Posts
15
Reaction score
12
Habari zenu wadau. Ikiwa zimebaki siku kadhaa kabla ya michuano ya AFCON kuanza nchini Misri naomba kujua kama King'amuzi au kituo chochote cha Luninga ambacho kitarusha Mubashara michuano hii hapa nchini( TANZANIA) ukizingatia tuna uwakilishi wetu kule wa timu yetu ya taifa.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Yaani hata Tibii-Sii nao chaliii?? wakat timu yetu ipo kule?? hili taifa haliko serious na michezo kabisa ![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tbccm vipi? Siku zote hizo watakuwa live Ikulu?
 
Kwa Azam, na startimes hawana leseni hiyo ila Kwese free channel zitaonyesha kwahyo
ni hivi TBC 1 itaonyesha gemu za Tz tu kupitia kwese free channel
kwahyo itakuwa hivyo hivyo kwa Kenya na Uganda kupitia nchi zao itaruhusiwa kuonyesha mechi kadhaa za timu zao tu hii ni kwasababu Azam wala startime hawakuomba reseni hiyo tofauti na Dstv ambayo imepewa leseni ya kurusha gemu zote
 
Daaaah Shukrani sana mkuu kwa maelezo yaliyonyooka. Wacha tuu tuwatafute DSTV walipo wasije wakatuongezea bei.
 
Kwa hiyo tutaangalia game mbili tatu tuu za awali kwa nchi yetu uhondo wa robo fainali na kuendelea hatutauona kupitia ving'amuzi vyetu pendwa. Ila na huu mfumo nao unatutesa sana walaji maana kila king,amuzi kina flavor yake yaani kwa style hii mtu unaweza ukajaza ving'amuzi ndani na TCRA wanatuangalia tuu kwa nn wasiweke mifumo rafiki kwa walaji ili tusijikute tunabeba mzigo mkubwa wa hizi huduma. Wana jambo la kufanya hapa kwa kweli vinginevyo itakuwa wanatutesa sana.
 
Back
Top Bottom