Kwa maoni yangu, katika viongozi tulionao sasa, ikiwa ni pamoja na wale walioko hivi ofisini na wale ambao tayari wamestahafu hakuna yeyote kati yao aliyetoa mchango mkubwa katika ustawi wa nchi yetu kama Aboud Jumbe.
Yeye ndiye aliyeipa Zanzibar katiba ya mwaka 1984. Kabla ya hapo, wananchi wa kawaida hawakuwa na sauti yeyote katika uendeshaji wa sauti yao. Madaraka yote ya kutunga sheria yalikuwa mikononi mwa Baraza la Mapinduzi ambalo wajumbe wake walikuwa wanateuliwa moja kwa moja na rais mwenyewe. Katiba hiyo ya mwaka 1984 ndiyo iliyoanzisha Baraza lawawakilishi.
Aidha bila ya Aboud Jumbe kuridhia kuunganisha ASP na TANU, CCM ambayo hivi sasa vigogo wengi wanajivunia hisingelizaliwa.
Katika hali hiyo, inakuwa vigumu kuelewa ni kwa namna gani mtu kama huyo, aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi ya yetu anavyoweza akaachwa kando na huku tukamtanguliza mtu ambaye japo amekuwa madarakani, lakini mchango wake ni ni wakutilia shaka.