Hoja yako naiunga mkono kwa saana tu.
Hakika kosa linodaiwa kufanya kumfanya huyu mzee wetu atumikikie jela maisha yote bila hata kukum bukwa kwenye PAROLE ya raisi siku za sikuku si kwamba labda alikwiba cha mtu wala kutenda kosa la kubaka oisipokua tu ni kwamba alidiriki kutenda kosa la KUENDEKEZA MAWAZO YA KIKATIBAKATIBA HIVI kwa enzi hizo ikawa taabu.
Na wala sitoshangaa endapo alichokiamini miaka hiyo kutumia mfumo wa serikali ya shirikisho kama ambavyo inavyotumika hivi sasa Marekani ikaja ikaonekana kuwa ni suluhisho bora zaidi wa namna ya kuboresha serikali kati ya bara na visiwani!!!
Na kwa sababu huyu 'mzee muona mbali' alidiriki tu kutenda kosa la kimawazo ambalo leo hii sisi wajukuu zake 'kosa' hilo hilo ndilo limekua wimbo mojawapo wa aina ya mabadiliko tunayotakataka kuona hapa chini ambao pengine huenda hata ikatuvuruga kabisa na baadhi ya wale ving'ang'anizi wenye fikra mgando wa mwaka wa 47, mie naona bora babu aachiwe huru mara moja, jeshi imjengee nyumba mahala atakapochagua na kupewa haki zake zote kwa utumishi uliotukuka kuliko kodi zetu zilazimishwe kuifanyia malipo kampuni za kitapeli kama Dowans.
Kwa kweli kwa uchungu mkubwa sana nami nimekua nikijiuliza mno kila ninapomuona huyu mzee wetu akisuguana bega na vibaka pale kwenye MV Alina akijikokota kwa shida kweli kweli na ligari la zamaniiii rangi ya krimu manjano hivi kila anapotoka au kurejea kule kifungoni kwake naanihii , si kule Robben Islandi; aggrr, samahani kule Kigamboni.
Hofu yangu tu ni kwamba kwa kuwa kule Pemba alizuiliwa kufika tangu zamani sana, leo hii ambapo kuna umeme mote huko alikozaliwa Pemba akirudi leo hii hatopotea kabisa vijiji?? Nyumbani jaamae, nyumbani kutamu hata kama ni misitu tuu!!
Je, endapo mtu yeyote mwenye dhamana atasikia sauti zetu dhaifu hizi lakini zenye nguvu kisirisiri, yule Mzee wetu MSTAARABU PEKEE WA SIASA NCHINI TANZANIA, Dr Ali Mohammed Shein, walau atajitolea vyombo vya usafiri wa aina zote kupereka ziarani hadi kule penye kilimo baharini huyu mzee wetu kuliko tu wanasiasa kuja kummiminia sifa za kinafiki baada mara baada ya kumsogelea muumba wake?
Je, Mwamnyanye ataona busara ozote kwenda na vijana wake kwenda kumjenge huyu mzee wetu mji kule Pemba kama ambavyo walivyomfanyia Mwalimu Nyerere kule Butiama badala ya kuja tu kusubiri mamba yaharibike kwa mzee wetu ndio waende KUPIGIA MIZINGA YA 'HESHIMA' kaburi???
Taifa letu linafuatilia kwa kiasi gani ustawi mzuri wa familia za wazee wetu wa bara na visiwani waliotutumikia hadi kuondoka ofisini bila KASHFA ZA UFISADI??? Wengi wao tunawaona mijini nyuso zao zikililia taifa hili KILAANA KABISA na hata kutoa taswira kama vile 'UADILIFU WANGU WA KUPIDUKIA KUTUMIKIA TAIFA LANGU NDILO LIMENIFIKISHA HAPA.
Mama yetu Anna Makinda, hebu iwekeni vizuri swala hili huko bungeni ili kodi zetu kuwasaidia waliotutumikia KIUADILIFU kusiwafikie tu kama hisani hisani vile. Mama nili ulimtembelea Prof Apiyo kwa mara ya mwisho? Mama Hawa Ngulume je, Banduka wako wapi na wanaongoza maisha ya aina gani, Joseph Rwegasira, Bob Makani, Edwin Mtei, Mama Shirima, Wazee wa Afrika Mashariki, familia ya Moses Mnauye, Bibi Titi, Mwalimu Nyerere, Dr Slaa, Chifu Mkwawa na wengine wengi tu??
Mama mbali na kazi bungeni tunataka kuona sura ya umama kweli na wakati wopte bila ubaguzi katika initiatives za kuyashughulikia haya.