Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kwenye underground wengi sana wanafanya makosa, hasa kwa vile wanatumia mbinu kama zako, kuchukua fundi abunibuni tu mchoro then vipimo vinaanza. Underground inahitaji planning nzuri ili interaction kati ya juu na chini iwe nzuri, wengine wanazitenganisha, yaani unakuta ili utoke underground uingie nyumba ya juu ni lazima utoke nje ndio uende ndani, while unaweza kuidizain vizuri ukapata kigorofa cha kishkaji.
 
Hiki ndicho kilichonikuta mimi mkuu, yaani haikuwa kwenye plan mwanzoni fundi alitegemea atajazia kifusi tu. Yaani kwa sasa hakipo kama chumba cha kulala kabisa kwanza hakina dirisha na hata huo mlango tulilazimisha kwa kuondoa baadhi ya tofali na umetoka mlango mdogo sana.
 
Kwani hizi haziwezi kukatwa???
Tatizo siyo kukata, hata uweke kitu kigumu vipi kama ni kukatwa kitakatwa tu. Tatizo ni kwamba flat bars wakivuta au kuzitwist na nondo/chuma zinaachia, wanaingia na kuiba tena ukiwa ndani umelala. Sasa nondo au square pipes mpaka wakate kutakuwa na kelele kiasi kwamba humo ndani mtasikia.
 
Dah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
"Sasa mwanzoni nilipanga yule wa kiume ndio atakuwa analala kwenye hiyo underground lakini ameniambia baba fanya ufanyavyo ila mimi sitalala huku bondeni kwenye banda la kuku akimaanisha ile underground."


....
Siku nyingine ukitaka kujenga,
Jipe muda kwanza wa kuitafakari ramani..
Heri upoteze muda kabla haujajenga,kuliko kujenga haraka ramani ambayo haujaridhika nayo.
 
Nyumba yako inafanana na nyumba Fulani huku mtaani ninakoishi
Au ndio hiyo?

Mwenye nyumba naye saa hii atakuwa anajutia.
Yeye hicho kichumba kiduchu Cha chini ameweka mpangaji,sijui anaishije mule maana ni kidogo,kimlango kiduchuu ila ni mwembamba anapita.
 
Kaka alaf balaa sqr 21300... mimi nyumba yangu ilihitaj sqrs 470 hiv jasho lilinitoka mzee [emoji28]
Hizi sqr 470 unamaanisha nini?
RM za bati?
Nyumba hiyo haizodi RM 350 mkuu.
Angalia kama ulipelekwa na fundi wamejiongezea RM za kutosha
 
Mkishapuliziwa zile dawa zao hamshtuki
 
Dirisha la jikoni kuwekwa baada ya kozi mbili ,matokeo yake wakati wa plumbing imekua ngumu kuweka sehemu ya sink, nimeingia hasara ya kutoa grill likakatwe na kupandisha kozi mbili tena ili kupatikane mahali pa kuweka sink la vyombo,sikutaka libanane kwenye kona

Fundi kutotoboa msingi ili nyumba ipumue,hapa nafikiria kutoboa hata kama nyumba imeshapanda.

Kujenga mashimo mawili ya choo badala ya moja,hii najutia mpaka kesho ,kila mtu site naona anajenga moja

Kupandisha kozi 11 badala ya 10 baada ya msingi,matokeo yake nyumba imekua ndefu sana
 

Ndefu ndo nzur mi nimejenga 11 lkn nimeona ya 12 nimepata wivu nyumba ndefu raha sana hasa kuanzia msingi
 
Hizi sqr 470 unamaanisha nini?
RM za bati?
Nyumba hiyo haizodi RM 350 mkuu.
Angalia kama ulipelekwa na fundi wamejiongezea RM za kutosha

Kaka bati nimenunua mwenyewe za kupima kihusu kuibiwa never mana mi alipima nikaagiza kiwandani fundi hakuusika kwa namna yoyote mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…