Nilisimamia ujenzi wa nyumba ya familia nikajifunza baadhi ya kanuni!!
1. Kugawanya ujenzi kwa phases, ambapo phase ya kwanza msingi, ya pili kupandisha na ya tatu kupaua hapo unakuja kwenye finishing hiyo ni phase ya nne yenye vipengele vidogo vidogo kama plambing, mabomba ya umeme, plasta, madirisha (grill) na n.k.
2. Kugawanya phases na kujengea mfukoni, unakwenda site na ramani yako unafanya makadirio na fundi ya gharama, nguvukazi na materials kwa phase ya kwanza. Unachofanya kadirio la fundi unaongeza na wewe kidogo (mafundi hawajui kukadiria). Unakusanya ile pesa.
3. Ukishakusanya pesa ya phase, unatafuta wiki au siku kumi za kazi ya phase 1. Mfano; ushaongea na fundi msingi utatumia siku nne, saa kumi na mbili upo site halafu wa mwisho kuondoka. Angalau utapunguza kupigwa na fundi na phase ya pili hivyo hivyo
4. Unapogawanya ujenzi kwa phase maumivu ni madogo sana. Mfano foundation m1.7 unatafuta m2 unasimamia show ukimaliza unaondoka na mahesabu ya kupandisha labda m4 unakwenda kuitafuta. Baada ya miezi ukirudi nyumba inapanda wiki tu mpaka inaisha japo ulisimama kwa miezi sita. Ukiondoka hapo na hesabu za kupaua na n.k.
NB: Ujenzi hakikisha unachorewa ramani tena mchoraji anafika site kuangalia eneo atakushauri vizuri sana