Ni kosa kubwa sana kumpa mwanamke uongozi kwani atategemea akili za wanaume kwa kila kitu

Ni kosa kubwa sana kumpa mwanamke uongozi kwani atategemea akili za wanaume kwa kila kitu

Mimi naamini hivyo,ukimpa uongozi mwanamke kwani atategemea kila kitu aamuliwe na mwanaume au wanaume.

Kibaya zaidi watamuamulia kwa maslahi yao kwanza hawatajali kama huyu mwanamke ataaibika,maana wanajua kwa kila aibu itajulikana aliyeamua ni huyo mwanamke


Kizuri mwanaume anapoamua jambo lake huwa hapendi kufanya vibaya kwa anayotaka kuyaamua ndiyo maana kabla ya kuamua hufikilia kwanza madhara na faida ya hilo jambo

Lakini mwanamke ni mtu wa kukurupuka huwa anaangalia kwa mda ule tu,na pindi jambo likishaharibika tu nafsi yake humuuma sana yuko radhi ajifungie ndani na asitoke inje


Hebu jiulize hivi Magufuli angekubali aruhusu yale yaliyotokea tarehe 29? Mimi naamini kuna watu walimshauri Hangaya ili yafanyike kwa maslai yao


Unajua Tanzania ilikuwa haijulikani kidunia kivile lakini imejulikana sababu ya yale mauwaji ya kutisha

Sijui mlioko madarakani mtaliponya vipi taifa maana badala ya kutafuta muafaka kwanza ndiyo mnazidi kuharibu

Ukitaka kujua watu wamezira angalia jinsi tume ya jaji Chande inavyokataliwa kupewa ushirikiano, vilevile kutokupewa sapoti kwa jambo lolote la kitaifa

Wazo langu kwa viongozi mtoeni Tundu Lisssu gerezani pamoja na wote wale wanaoshikiliwa

Na wasiojulikana itisheni mjadala wa kitaifa, wawajibishwe wote waliofanya mauaji, paitishwe serikali ya mpito au mama jiuzuru ili uponye nafsi yako.

Naamini Tanzania itarudi kwenye mstari wake bila hivyo tusubirie anguko jingine baya kabisa linalokuja mbele yetu
Sisi Waafrika, na Watanzania kwa ujumla, tulifundishwa tangu zamani kuwaheshimu wafu na waliotangulia mbele za haki. Ndiyo maana maeneo ya makaburi yamekuwa yakichukuliwa kuwa ni sehemu takatifu na zinazoheshimiwa sana katika tamaduni za Kiafrika.Kitendo cha baadhi ya viongozi wa juu wa nchi kuwadhalilisha watu waliofariki tarehe 29, kuwazika katika makaburi ya halaiki, na wengine kuchomwa katika viwanda vya saruji, ni kosa kubwa sana lisilokubalika kijamii, kiutu wala kiimani. Kwa mtazamo wa kiroho, hatua hizi zimeiacha nchi katika hali ya laana nzito. Inasikitisha kuona wazee wetu, ambao walipaswa kuwa walinzi wa maadili na hekima ya taifa, wakishangilia kejeli zilizotolewa dhidi ya wale wote waliouawa siku ya maandamano. Taifa hili limejeruhiwa kimaadili na kiroho, linahitaji kutafakari kwa kina, kufanya toba ya kweli, pamoja na maombi na sadaka kubwa.
 
Huyu ndiye mwanamke wa mwisho Tanzania kuikalia ikulu . Hata bibi wa Gen Z alishauri hilo
 
Unajitahidi sana kumchafua Rais SSH lakini kuna mahali hoja yako inaanza kuwa nyepesi.

Kumbuka ile hotuba aliyoitoa hayati JPM kuhusiana na maandamano alipowapiga mkwara kina Mbowe kwamba wasiandamane. Akiwaambia watangulie kwanza wao.

Maana yake ni kwamba wangeandamana wangekutana na kipigo cha aina ile ile ya tarehe 29 October bila kujali uanamme wake au uanamke wa SSH.

Kumbukeni urais ni taasisi sio shughuli ya mtu mmoja, pale ikulu kuna wasaidizi wengi kwenye fani mbalimbali, ukiona anaongea mbele ya kamera ujue ni maamuzi ya taasisi sio ya mtu mmoja.

Mnaongozwa na dhana ya chuki yenye ubaguzi ndani yake kwamba JK ndiye anayemuongoza Samia, JK hutoa ushauri pale inapobidi haswa Samia awe yeye mwenyewe anataka ushauri wa JK ndio atamfuata na kumuomba.

Kuna wasomi wengi wenye uwezo mkubwa wapo nyuma ya Samia, huwezi kulinganisha anayoyafanya kiuchumi na yale waliyoyafanya marais waliopita.
SWali dogo, inamaana hao wasomi washauri wa samia ndio kabisa na akili zao timamu wamemshauri amteue mwanae wa kumzaa kuwa naibu waziri achilia mbali mkwewe?!

Najua katiba haijakataza, lakini hekima na busara inagoma...ndio maana hakuna rais yeyote aliyemtangulia amewahi kufanya ujinga huo!

Kwakifupi, Samia hatoshi kwenye urais...katiba imetuangusha sana kwa kuruhusu huyu mama kuwa rais wetu japo kwa njia za mchongo!
 
SWali dogo, inamaana hao wasomi washauri wa samia ndio kabisa na akili zao timamu wamemshauri amteue mwanae wa kumzaa kuwa naibu waziri achilia mbali mkwewe?!

Najua katiba haijakataza, lakini hekima na busara inagoma...ndio maana hakuna rais yeyote aliyemtangulia amewahi kufanya ujinga huo!

Kwakifupi, Samia hatoshi kwenye urais...katiba imetuangusha sana kwa kuruhusu huyu mama kuwa rais wetu japo kwa njia za mchongo!
Nenda Uganda uone Museveni alivyowapa vyeo nyeti ndugu zake punguza kulialia.

Samia anatosha sana ongea kwa data na takwimu sio kwa hizi chuki za kipuuzi.

Samia kamaliza miradi yote aliyoachiwa na hayati JPM hivi sasa anajenga miradi yake. Nchi inao utulivu.
 
Back
Top Bottom