Ni kosa Wakristo kuwa matajiri?

Ni kosa Wakristo kuwa matajiri?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nimeshasikia mara kadhaa mahubiri yenye maneno yanayofanana na haya:

1. "Ole wenu wahubiri mnaowahubiria watu uponyaji na mafani"

2. "Makanisa ya siku hizi yanahubiri mafanikio tu"

3. N.k.

Ni kosa Wakristo kufundishwa jinsi ya kufanikiwa kifedha na kuwa na afya njema?

Kuna ubaya wo wote kwa Mkristo kuwa tajiri?
 
Sadaka hizi hizi ndio zinawanunulia wachungaji v8 huku waumini hata kula yao ya shida
 
Nimeshasikia mara kadhaa mahubiri yenye maneno yanayofanana na haya:

1. "Ole wenu wahubiri mnaowahibiria watu uponyaji na mafanikio"

2. "Makanisa ya siku hizi yanahubiri mafanikio tu"

3. N.k.

Ni kosa Wakristo kufundiahwa jinsi ya kufanikiwa kiafya na kifedha?

Kuna ubaya wo wote kwa Mkristo kuwa tajiri?
Utajiri ni majaaliwa ya Mungu kwa mwanadam Wala hayapaswi kuhubiriwa,Yesu alisema maskini mnao siku zote Mimi hamnami siku zote!

Kwa hiyo mahubiri ya utajiri hayana mashiko coz sio Mpango wa Mungu watumishi wahubiri hayo,wao Wana paswa wahubiri toba ya dhambi na utakatifu pia kufanya kazi kwa bidii na kuacha dhambi hayo ya utajiri ni mapenzi ya Mungu mtu awe na sio lazima utajiri uwe kipimo Cha ukristo! mahubiri ya utajiri waachiwe inspiration speakers ndio jukwaa lao sio watumishi wa Mungu!!!

Nimejitahidi! Kueleza!!
 
Mkristo kuwa masikini ni laana.
Torati 28.
Yesu ametukomboa na laana za torati.
 
Nimeshasikia mara kadhaa mahubiri yenye maneno yanayofanana na haya:

1. "Ole wenu wahubiri mnaowahubiria watu uponyaji na mafani"

2. "Makanisa ya siku hizi yanahubiri mafanikio tu"

3. N.k.

Ni kosa Wakristo kufundishwa jinsi ya kufanikiwa kifedha na kuwa na afya njema?

Kuna ubaya wo wote kwa Mkristo kuwa tajiri?
Kuwa tajiri sio kosa
 
Mchungaji na awe wa kwanza kujiombea apate utajiri,
Akishaupata awahubirie na awaombee kondoo wake pia!
Haiwezekani, mwenyewe aombe sadaka za waumini ili awe tajiri Ila waumini awaambie watapata utajiri kwa maombi!
Hapo ndipo panaleta ukakasi kuhusu mahubiri na maombi ya utajiri!
 
Back
Top Bottom