Ni Kristo au Kristu?

Ni Kristo au Kristu?

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,802
Reaction score
3,253
Habari ya wakati huu

Naomba kuuliza maana hiki kitu kinanichanganya sana. Sijui kichwa changu ndio kigumu.

~Ni Yesu Kristu au Yesu kristo
~Je, dini ni Mkristu au Mkristo

Naombeni majibu tafadhali

AHSANTENI.
 
Ngoja waje akina Pasta Mashimo kukupa Muongozo.
 
Kwa uelewa wangu
Kristu, hii ni kwa Roma
Kristo, hii kwa madhehebu mengine
 
Zote sawa...

Moja ni tafsiri ya kilatini kwenda kiswahili... Cristus....kristu

Nyingine ni tafsiri ya kigiriki kwenda kkiswahili Christos.....Kristo..

Mfano.. Kilatini....Augustus
..Kigiriki...Augustos

Kwakifupi lagha za biblia ni kilatini na kigiriki... Majina ya kilatini lazima yamalizikie na ....US na kigiriki yanamalizikia na ...OS
 
Hapana.. hizo ni lugha ... Utasikia sana kwa Wakatoliki wakitumia Kristu kwakuwa lugha ya rasmi ya kanisa katoliki ni kilatini
Mbona nimemsikia padre mmoja radio tumaini anasema Yesu kristo.
 
Habari ya wakati huu

Naomba kuuliza maana hiki kitu kinanichanganya sana. Sijui kichwa changu ndio kigumu.

~Ni Yesu Kristu au Yesu kristo
~Je dini ni Mkristu au Mkristo

Naombeni majibu tafadhali

.....................AHSANTENI...................
Majibu yako kwenye biblia mkuu.Ukikuta pahala kwenye biblia wameandika KRISTU,ujue hiyo biblia ni fake
 
Zote kilatini na Kigiriki ni lugha za kanisa....Kwa namna ya kipekee Kilatini kimepewa kipaumbele
Lugha za Kanisa tena[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787] lugha ya wagiriki wapagani wa nyota 5 unakuwa ya Kanisa mbona una sound kama watoto wa Mudi na slogan yao kuwa kiarabu ni lugha Ya Allah
 
Lugha za Kanisa tena[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787] lugha ya wagiriki wapagani wa nyota 5 unakuwa ya Kanisa mbona una sound kama watoto wa Mudi na slogan yao kuwa kiarabu ni lugha Ya Allah
Kuna uhusiano gani kati ya lugha na upagani?
 
Kwahiyo Kanisa ikajichagulia lugha ikawa ya kwao
Kuna sababu kadha wa kadha zimetumika.. Moja ni kuwa lugha za kilatini na kigiriki ni kongwe na zina misamiati mingi.. Hivyo ili kuhifadhi mafundisho ya kanisa yasije yakabalishwa au kupotoshwa maana halisi lugha kongwe hizi lazima zitume..

Leo hii kuna tafsi nyingi za kimaandiko mpka zingine zimefikia hatua za kupotosha maana halisi ya kilichokusudiwa... ndio maana ili kujua maana halisi ya kilicho andikwa lazima urudi kwenye maandishi ya lugha mama za biblia yaanni kilatini na kigiriki..
 
Back
Top Bottom