Ni Kupuuzia au ni mfumo dhaifu ktk uhitaji wa ushauri wa kitaalam?

Ni Kupuuzia au ni mfumo dhaifu ktk uhitaji wa ushauri wa kitaalam?

The BornAgain

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2024
Posts
463
Reaction score
649
Habari wanajamvi?

Watanzania wengi hawapendi sana ushauri kitaalamu kuhusu kuendesha au kuanzisha miradi yao au biashara zao!! Angalau kidogo kwenye mambo ya sheria muamko upo, na kwenye mahesabu angalau, lakini mwambie mtu andika au andikiwa huo mradi/biashara au shauriwa kabla hujaanza au wakati unaendelea wengi hawavutiki, hawako tayari haijalishi ukubwa wa mradi au biashara.

Ushauri ni jambo mhimu kabla kuanzisha na wakati wa kuendesha biashara/mradi!! TATIZO NINI? Mengine wanaona kupoteza muda, wengine wanaamini nguvu ya pesa kama tayari wanazo, wengine wanadharau wataalam husika, wengine wanaegemea ushauri kirafiki na kijamaa, kuiga, nk.

Hivyo wasomi wengi ktk nyanja hizo kujikuta hawana ushawishi, lakini moja ya sababu ya biashara au miradi kufeli kufikia malengo yake ni ukosefu wa ushauri wakati wanaanza au hata wakati wanaendesha maana biashara ikiugua ni kama binadamu vema akawaona madakitari, lakini kama ilivyo hata ktk afya wengi sisi tunakimbilia kujitibu wenyewe kwa ujuaji, uzoefu na ushauri kwani hatutaki kuwaona madaktari eti kisa kutaka kusave pesa ya kumuona daktrari! Lakini wachache wanaheshimu washauri waelekezi ktk nyanja zao za utaalam.

Himizo ni kuwa vema inapobidi tutumie wataalamu wetu ktk mahitaji kadha wa kadha, sababu hatujui kila kitu. Tusingoje tuharibikiwe kisa kuepuka gharama zao, sometimes tunaweza epuka gharama zaidi za baadae au kupunguza risks nk.
 
Back
Top Bottom