Ni kwa kiwango gani maamuzi unayoyaita “maamuzi yangu” kweli hayo ni yako?

Ni kwa kiwango gani maamuzi unayoyaita “maamuzi yangu” kweli hayo ni yako?

Joined
Feb 28, 2022
Posts
84
Reaction score
84
Hukuchagua kuzaliwa.

Hukuchagua mwili uliopewa.

Hukuchagua ubongo ulio nao.


Lakini cha kushangaza ni kwamba, karibu kila uamuzi unaoufanya maishani hutoka kwenye ubongo huo huo - ambao huenda hukuwekeza muda wa kutosha kuujenga, kuufundisha au kuhoji namna unavyofikiri.


Basi jiulize:

Ni kwa kiwango gani maamuzi unayoyaita “maamuzi yangu” kweli hayo ni yako?

Ni kiasi gani cha maisha yako kinaongozwa na mazoea, malezi, mazingira, hofu, tamaa, majeraha ya zamani, shinikizo la jamii na imani ulizorithi bila kuzipima?


Na ni kwa kiwango gani umeanza kusimama pembeni ya fikra zako, kuziangalia, kuzihoji na kuchagua kwa uangalifu kile unachotaka kuamini na kutenda?


Huenda uhuru wa kweli si kuishia kufanya kila unachotaka.

Huenda uhuru wa kweli ni kuweza kuutambua mfumo unaokufanya utake kile unachotaka.


Tafakari:
Kama usingehoji fikra zako, ungewezaje kujua kwamba kweli wewe ndiye unayeamua?...
 
Tuko kwenye mtihani, kila mtihani una maelekezo yake, wewe unachofanya wewe ni kuhoji maelekezo ya mtihani wako kama yako sahihi au la
 
Back
Top Bottom