Ni kwa namna gani nzuri naweza kuishi na mama mzazi asiyeniheshimu?

Ni kwa namna gani nzuri naweza kuishi na mama mzazi asiyeniheshimu?

Tetra fino

Member
Joined
Jul 13, 2026
Posts
26
Reaction score
44
Good afternoon Wana jamii forums,

Poleni na hongereni kwa majukumu.
Mimi ni mwanamke miaka 47 single Maza wa watoto wawili ,Mume wangu alifariki miaka miaka mingi imepiata ila kabla ya kufariki tulikua tushatengana.

Kilichonileta kwenu ni kuwa baada ya yeye kufariki nilirudi nyumbani kuishi na wazazi Ili niweze kujijenga upya kiuchumi, kwani hakukua na chochote alichoacha marehemu Mume wangu.

Ila tokea naishi na wazazi wangu wamekua n watu wa kunidharau, kunisema vibaya kwa ndugu hata mbele ya wanangu hadi wanangu wananidhau Mimi mama yao.

Kuhusu biashara najishughulisha na biashara ndogondogo ambayo haikidhi mahitaji ya wanangu hvyo bibi yao huwa anawalipia ada mimi natoa matumizi.
 
Anza kuwajibika kwa yote yanayokuhusu kwa 100% . Hii sio ngumu, fanya mambo kulingana na uwezo wako ili upunguze utegemezi kwa watu. Mwanadamu ana kawaida ya kuchoka kutegemewa, hata awe ndugu wa damu. Utamlaumu bure!
 
Wala usimlaumu mama yako
Mzigo wa watu 3 si mchezo,kwa umri huo ulipaswa uwe kwako huwezi kuishi chini ya amri ya mtu wingine kila kitu utakuwa unalalamika tu
Nimejaribu kutafuta kazi mara kadhaa Ili nikae mbali na nyumbani lakini amekua akilalamika anahitaji uangalizi wa karibu sababu anaumwa pressure na miguu hvyo hawezi kuishi mwenyewe
 
Nimejaribu kutafuta kazi mara kadhaa Ili nikae mbali na nyumbani lakini amekua akilalamika anahitaji uangalizi wa karibu sababu anaumwa pressure na miguu hvyo hawezi kuishi mwenyewe
Huyo mzazi wako ni umri unamsumbua tu! hata bibi yangu ana hiyo tabia kabisa! kuna muda anataka kukaa mwenyewe kuna muda anataka watu, haeleweki! mvumilie tu! watoto wako watengenezee mipaka wala hawatakudharau.. we deal na wanao tu!
 
Pole sana kwa changamoto, kuna kitu kidogo sana haujakielewa , kuendelea kuwepo nyumbani kwa wazazi hasa kwa age yako wewe ni kupoteza status ya utu uzima wako, utaendelea kuonyeshwa dharau kwa sababu tayari ameshagundua hauna msaada wowote, wewe ni tegemezi.

Cha kufanya usiwe mtu wa kukaa nyumbani, kuwa mtu wa mikakati hata kama hauna dira kwa sasa, usiwe available sana nyumbani, naamini hauwezi kukosa cha kufanya nje.

Usiruhusu kuonyeshwa dharau mbele ya watoto wako, ukishaona dalili za kudharauliwa au kusemwa ukiwa na watoto wako, nyanyuka wachukue wanao utoke nao kwa heshima tu, wala usiwaonyeshe kuwa umechukia , kuwa normal.

Wewe ni mtu mzima, itapendeza kama utakaa na mama na kumueleza anachokifanya hakikufurahishi , toa yote ya moyoni ukiwa kwenye utulivu.

Soma ni wakati gani maalum au tukio gani hasa ambalo mama yako anatumia kukudharau zaidi ,ni mbele ya ndugu, au mbele ya watoto wako?

Ukishagundua jitahidi kutokuwa karibu yake kwa namna yoyote ile muda huo.
 
Ndio ila bibi yao anataka wamalize chuo wapate vyeti,n
Vyeti vipo vya aina nyingi, taaluma mbalimbali. Msilazimishe watoto mambo wasiyoyamudu!
Somesha vijana masuala ya hotel, utalii, ufundi ujenzi, seremala, mabomba , gereji udereva, ufundi kompyuta, programming, mapishi ya keki na vitafunwa, mapambo, n.k. atapata vyeti na ujuzi na ajira ni nyingi ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom