Ni kwa nini matajiri wengi wa Dunia wanatoka Marekani?

Ni kwa nini matajiri wengi wa Dunia wanatoka Marekani?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nimejaribu kupitia 'list' ya matajiri duniani, nikagundua wale ma-top wengi wanatoka Marekani.

Ukiangalia ata wasanii wao au wafanya biashara kutoka huko kwao wanamiliki ndege n.k

Sasa najiuliza, ni kitu gani kinacho wafanya wao kuwa na matajiri wengi.

Ni kwamba wana sera nzuri za kuwawezesha raia wao kuwa matajiri, au wanawakopesha, au kuna namna nyingine?

Njooni tujadili.​
 
Marekani na nchi zingine za Magharibi kuna Uhuru mkubwa sana wa mtu kuweza kutumia akili zake, nguvu zake na uwezo wake alionao vizuri zaidi katika kujitafutia kipato halali. Mazingira yanaruhusu, Demokrasia husababisha kuwepo kwa Uhuru mpana zaidi wa watu kujiamulia mambo yao, huleta Uhuru wa fikra.

Mifumo ya Utawala katika nchi za ki-Afrika haitoi nafasi kabisa kwa mtu yoyote yule raia wa kawaida kuweza kuonyesha kipaji chake, karama yake au ujuzi wake alionao to the fullest.

Ukiwa upo katika nchi za Afrika Kama vile Tanzania, ukifanya ugunduzi mpya wa kitu Kama vile kutengeneza bunduki ya kisasa, utakamatwa na kwenda kufungwa jela badala ya kuajiriwa na/au kupelekwa Jeshini ili uende ukazalishe au kutengeneza bunduki nyingi zaidi kwa matumizi ya Jeshi katika shughuli zake za kiulinzi.
 
Back
Top Bottom