Ni kwa sababu gani BRICS inavutia sana Dunia ya Kusini?

Ni kwa sababu gani BRICS inavutia sana Dunia ya Kusini?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1729752313633.png

Mkutano wa kilele wa BRICS umefanyika kuanzia Oktoba 22 hadi 24 huko Kazan, nchini Russia, ukiwa ni wa kwanza baada ya kundi hilo kuongeza nchi wanachama, na hivyo kufuatiliwa sana na jamii ya kimataifa.

Kundi la BRICS, ambalo ni kifupi cha majina ya nchi zinazoibuka kiuchumi na senye matarajio mazuri ya kiuchumi, lilianzishwa na nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, na sasa limebadilika na kuwa mfumo wenye ushawishi mkubwa wa ushirikiano wa kimataifa, ambao pia umeongeza idadi ya nchi wanachama. Licha ya nchi ambazo zimejiunga rasmi na BRICS Januari Mosi mwaka huu, zaidi ya nchi 30 zikiwemo Thailand, Malaysia, Uturuki na Azebeijan aidha zimeonyesha nia ya kuwa wanachama wa kundi hilo, na hivyo kufanya ushawishi wa BRICS kuendelea kuwa mkubwa duniani.

Benki Mpya ya Maendeleo (NDB) iliyoanzishwa na BRICS, inalenga kukusanya rasilimali kwa ajili ya miundombinu na miradi ya maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa kundi hilo na nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na nchi zinazoendelea. Benki hiyo yenye makao makuu yake mjini Shanghai, imepitisha jumla ya mikopo yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 35 kwa ajili ya miradi karibu 100, ukiwemo mrasi wa Umeme wa Upepo wa Serra da Palmeira wa nchini Brazil, na Mradi wa Ugavi wa Bidhaa za baridi wa Jiangxi Mjini na Vijijini nchini China.

Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amesema, ushirikiano wa BRICS umekuwa na manufaa dhahiri kwa nchi hiyo katika sekta mbalimbali. Pia ameeleza kuongezeka kwa biashara kati ya Afrika Kusini na nchi nyingine wanachama wa BRICS, na fedha zilizotolewa na Benki Mpya ya Maendeleo kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za ndani. Amesema thamani ya jumla ya biashara kati ya Afrika Kusini nan chi nyingine za BRICS imeongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 27.67 mwaka 2017 hadi dola za kimarekani bilioni 39.89 mwaka 2021.

Nchi mpya wanachama wa BRICS zimeonysha shauku ya kuboresha maendeleo yao ya uchumi kupitia mfumo huu wa ushirikiano. Mkuu wa Umoja wa Wawekezaji wa Kiarabu wenye makao yake makuu mjini Cairo, Misri, Gamal Bayoumi anasema, uanachama wa Misri katika BRICS utaiwezesha nchi hiyo kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka NDB badala ya kukopa fedha yenye riba ya juu kutoka kwenye benki nyingine za kimataifa.

Mshauri wa mawasiliano na machapisho katika Taasiai ya Elimu ya Sera nchini Ethiopia, Balew Deissie anasema, uanachama wa Ethiopia unaweza kuwezesha ushirikiano wa kina zaidi wa Kusini na Kusini, na kuiwezesha nchi hiyo kuboresha upatikanaji wa masoko mbalimbali ya kimataifa na teknolojia. Pia anasema, nchi za BRICS zinaipatia Ethiopia jukwaa la kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja wa kigeni kwa kutumia nguvukazi yake ya vijana, na utajiri mkubwa wa maliasili.

Tangu kuanzishwa kwake, nchi wanachama wa BRICS wamejikita katika kudumisha uhusiano wa pande nyingi na kuwa nguvu chanya na tulivu katika masuala ya kimataifa. Baada ya kuongeza nchi wanachama, hivi sasa kundi la BRICS linachukua karibu asilimia 30 ya pati la jumla duniani, na idadi ya watu katika mfumo huo ni karibu nusu ya watu wote duniani, lakini pia, biashara kati ya nchi wanachama wa kundi hilo inachukua moja ya tano ya biashara duniani. Kutokana na kukua kwa ukubwa wa kiuchumi na kuongezeka kwa diplomasia ya kivitendo, nchi wanachama wa BRICS wanaongeza hatua kwa hatua ushawishi wao katika mchakato wa kimataifa wa kufanya maamuzi.

Nchi nyingi za Dunia ya Kusini zinatafuta utaratibu mbadala wa dunia kuliko uliopo sasa, ambao umetawaliwa na mkusanyiko wa wenzi unaoongozwa na Marekani na unaokosolewa kwa masuala ya utengano wa siasa za kijografia. Nchi hizo zinaangalia nchi wanachama wa BRICS kuzisaidia kupaza sauti zao kwa suala linalopuuzwa la haki zao za kimsingi za kujiendeleza.
 
Katika jambo linalonifanya niunge mkono BRICS ni kuleta balance of power, hakuna tena mambo ya dunia kuendeshwa na West.

Long live Putin.
Kabisa,wale mbwa wa west roho mbaya sana, vikwazo korea kaskazini vya nini?..watu wafa njaa,maisha magumu, vikwazo cuba vya nini na fidel hayupo!?.. venezuela wameihujumu kisa hawajawapa mafuta yao
 
Kabisa,wale mbwa wa west roho mbaya sana, vikwazo korea kaskazini vya nini?..watu wafa njaa,maisha magumu, vikwazo cuba vya nini na fidel hayupo!?.. venezuela wameihujumu kisa hawajawapa mafuta yao
Mgogoro wa Ukraine umetufumbua wengi macho Mkuu, hapo kabla nilishajazwa propaganda za West juu ya Putin, Xi Jinping na Kim.

Lakini kwa sasa najua ukweli ni upi. Iran kuingia BRICS nimefurahi sana.
 
World bank na IMF ni vyombo Kwa jina la taasisi za UN,lakini kiukweli vimekua ni fimbo ya kuziadabisha nchi zinazotofautiana na mabeberu.
Mabebebru hawaheshimu kabisa tamaduni za nchi nyingine,watawaambia mfuate masharti Yao ili mpate huduma za WB na IMF.
Lakini ukiangalia masharti
hayo utakuta yanapingana kabisa na tamaduni zenu,
mkiyakataa masharti hayo IMF na WB watahusika kuwaadibisha.
Sasa BRICS ndio jibu la kero hiyo.
Mabebebru wasiogope wainywe TU hata kama ni chungu kwa sababu ujio wa BRICS ni aina ya demokrasia,yaani Ukiona WB na IMF wanazingua unaenda kwa BRICS bank.
 
Mgogoro wa Ukraine umetufumbua wengi macho Mkuu, hapo kabla nilishajazwa propaganda za West juu ya Putin, Xi Jinping na Kim.

Lakini kwa sasa najua ukweli ni upi. Iran kuingia BRICS nimefurahi sana.
Nawapenda sana wadada kama wewe.
Simaanishi kimwili,Bali kiroho.
Kwa sababu Una upeo Mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom