Ni kwanini ccm wana upendo mkubwa kwa Freeman Aikaeli Mbowe?

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam

Nimekua nashangaa sana kila kukicha viongozi wengi wa ccm wanataka mbowe awe mwenyekiti wa chadema wa kudumu. Najiuliza tu huu ni upendo wa dhati au ni mahaba? Je huenda ni kweli zile tetesi kwamba mbowe ni pandikizi la ccm kuidhoofisha chadema ili isishike dola?

Maana kuna kampeni ccm wanapiga chinichini kwamba tundu lissu asikabidhiwe chama eti atakivuruga na kukisambaratisha, inashangaza huu upendo wa ccm kwa chadema kwamba isisambaratike. Hapa nilitegemea ccm wamfanyie kampeni TL ili awe mwenyekiti na akaisambarishe chadema ili wanufaike.
 
Wasalaam

Nimekua nashangaa sana kila kukicha viongozi wengi wa ccm wanataka mbowe awe mwenyekiti wa chadema wa kudumu. Najiuliza tu huu ni upendo wa dhati au ni mahaba?
Ni upendo wa dhati
Je huenda ni kweli zile tetesi kwamba mbowe ni pandikizi la ccm kuidhoofisha chadema ili isishike dola?
sii kweli
Maana kuna kampeni ccm wanapiga chinichini kwamba tundu lissu asikabidhiwe chama eti atakivuruga na kukisambaratisha,
ni kweli
inashangaza huu upendo wa ccm kwa chadema kwamba isisambaratike.
ni kweli CCM hatutaki chadema isambaratike ili tupate chama cha kupokezana
Hapa nilitegemea ccm wamfanyie kampeni TL ili awe mwenyekiti na akaisambarishe chadema ili wanufaike.
No!
Tena Mkuu Princess Subi, Subira the princess , hata mimi ni CCM na nampenda Mbowe Kuelekea 2025 - Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila...
p
 
Tofauti na unavyosema CCM ndio mnaofanya kila juhudi Mbowe akataliwe na wanachama wenzake. Mara, amepwaya ile nafasi apewe Heche au Lissu. Mara amekaa muda mrefu mno na sasa panahitajika damu changa. Hii ya kwako ni uendelezo ule ule wa kuleta fitna kuwa Mbowe ni kipenzi chenu hivyo haaminiki.
Kwa kweli mnachosha. Mbowe ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema mpaka mojawapo ya vifuatavyo vitokee:
1. Mwenyezi Mungu amfanye asiweze kuendelea na cheo hicho.
2. Mwenyewe aamue kuwa hataki kuendelea na cheo hicho.
3. Wanachama wa Chadema waamue kumpumzisha.

Fitna zenu haziwezi kufanikiwa. Badala ya kuendelea kuifuatilia CDM, kazaneni kutatua matatizo ya wananchi ili msilazimike kucheza foul kwenye uchaguzi,

Amandla...
 
Wasalaam

Nimekua nashangaa sana kila kukicha viongozi wengi wa ccm wanataka mbowe awe mwenyekiti wa chadema wa kudumu. Najiuliza tu huu ni upendo wa dhati au ni mahaba? Je huenda ni kweli zile tetesi kwamba mbowe ni pandikizi la ccm kuidhoofisha chadema ili isishike dola?

Maana kuna kampeni ccm wanapiga chinichini kwamba tundu lissu asikabidhiwe chama eti atakivuruga na kukisambaratisha, inashangaza huu upendo wa ccm kwa chadema kwamba isisambaratike. Hapa nilitegemea ccm wamfanyie kampeni TL ili awe mwenyekiti na akaisambarishe chadema ili wanufaike.
Tofauti na unavyosema CCM ndio mnaofanya kila juhudi Mbowe akataliwe na wanachama wenzake. Mara, amepwaya ile nafasi apewe Heche au Lissu. Mara amekaa muda mrefu mno na sasa panahitajika damu changa. Hii ya kwako ni uendelezo ule ule wa kuleta fitna kuwa Mbowe ni kipenzi chenu hivyo haaminiki.
Kwa kweli mnachosha. Mbowe ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema mpaka mojawapo ya vifuatavyo vitokee:
1. Mwenyezi Mungu amfanye asiweze kuendelea na cheo hicho.
2. Mwenyewe aamue kuwa hataki kuendelea na cheo hicho.
3. Wanachama wa Chadema waamue kumpumzisha.

Fitna zenu haziwezi kufanikiwa. Badala ya kuendelea kuifuatilia CDM, kazaneni kutatua matatizo ya wananchi ili msilazimike kucheza foul kwenye uchaguzi,

Amandla...
Haaminiki hata kidogo
 
Back
Top Bottom