Ni kwanini hatumuelewi Mzee Magoma?

Ni kwanini hatumuelewi Mzee Magoma?

Huyu mzee ovyo sana avuliwe uanachama na mkutano mkuu wa wanachama kwa kuleta sintofahamu. Siku zote alikuwa wapi wakati Yanga ikitembeza bakuli na kufungwa na Simba.

Hawa wazee hawaendi na wakati si ajabu bado anaamini Rais bado ni Nyerere!!

Njaa kali inamsumbua tu atafute chaka jingine sio Yanga! Kwani mapori si yamejaa akalime mpunga huko Moro.

Hawa ndo virusi na mamluki wa kolowizard lazima atolewe klabuni haraka, kuendelea kumchekea itaharibu soka letu na akili zake za kwenda mahakamani zinaweza kusababisha nchi nzima kufungiwa na FIFA kushiriki michuano ya kimataifa.
Anadai timu ile ni ya watu maskini, GSM inawapora timu yao, yani wao akina magoma ndio timu yao..na kwamba migogoro ni chakula cha timu..yani binafsi naelewa kuwa hizi kariakoo clubs zilianzishwa kwa mazingira fulani kisiasa ivi, nk..sasa wawekezaji wanapoingia hawa wenye timu kiasilia wanachukia mtindo wa uendeshaji..Eng herse ni kijana hakuwepo Yanga ikianzishwa miaka hiyo anasoma historia tu lakn pia mashabiki wengi waliopo sio wale wa wakat wa magoma, hivyo basi Eng anaendesha timu kufuata uhalisia wa sasa wa kisasa..ndio mana mm na wengine wa sasa tunaona Magoma hana POINT japo wale wa zaman wanaona ana Point..hali kadharika Simba nako kuna wengine walimchukia MO kwa kuwaweka mbali wazee sabb zinafanana fanana..yani migogoro kwa hizi timu mbili hutengenezwa makusudi nadhani ni sehemu ya falsafa yao mmoja awe chini mwingine juu..yani isitokee yanga na simba wote wako sawa kiuchumi na kiuongozi..ndo sasa bila mgogolo yanga simba itastruggle sana kupata ubingwa mbele ya yanga hata was ajili vizuri..ndo mana unaona mara GSM anadhamini timu 6 mara MO weka hizo B20 tuone..yani mkanyagano..sasa wazee kwa wazee huko wamekaa wakaona ukisasa sio..vuruga tu tuanze mwanzo..yanga ilikuwepo tangu enzi na itaendelea hata bila GSM au simba bila MO..wako sahihi lakn wanaharibu mood zetu mashabiki wa juzi. Sorry
 
Back
Top Bottom