Ni kwanini kila mzigo anapewa Rais?

Ni kwanini kila mzigo anapewa Rais?

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Hivi Watanzania wanaelewa mifumo ya uongozi? Kama hawaelewi huko shuleni wanajifunza nini? Kila Jambo hata Mambo madogo ya kifamilia utasikia mtu anamlilia Rais.

Mtu akitembea na mke wa mtu akikamatwa utasikia Mama yetu tusaidie haki itendeke😆
Mtu akinyimwa kitu utasikia anamlilia Rais.

Serikali au Rais haiwezi kushughulika na kila kitu hata Mambo ya kifamilia, mtatuzi wa mwanzo wa changamoto niwewe mwenyewe, Watanzania pelekeni hoja nzito kwa Raisi sio kila Jambo mnasema mama mama
 
Rais mwenyewe ndio anapenda hivyo, kwani hicho ndio kipimo halisi cha kujua watu wamelala kwa kiasi gani.
 
Hivi watanzania wanaelewa mifumo ya uongozi? Kama hawaelewi huko shuleni wanajifunza Nini? Kila Jambo hata Mambo madogo ya kifamilia utasikia MTU anamlilia Rais...
Kama taifa tulikosea kukuza majina ya watu kuliko taasisi!!

Yaani state yetu iliruhusu majina yawe makubwa kuliko taasisi za jamhuri yetu!

Matokeo yake majina makubwa hufa na kutuachia uozo kwenye taasisi zetu!

Ndio maana watu wanaliita jina la Rais kwenye Kila kitu badala ya kutatuliwa matatizo Yao na taasisi husika!!

Mandela,kwame nkuruma, Nyerere na mashujaa wore wamekufa na majina makubwa lakini wameacha taasisi mbovu na matatizo kibao tuliyonayo Hadi leo!!
 
Mvua ikinyesha mama anaupiga mwingi, sasa kwanini jua likiwa kali asitajwe na yeye.

Uchawa wenu ndio unaleta yote haya. Ukiingia airport mpaka mjini mmetandaza mabango ya mama anaupiga mwingi.

Mlishamfanya kama demi god, ni cult mmemtengenezea sasa kama vile anavyopewa sifa asizostahiki basi kubalini anapopewa lawama pia.
 
Hivi watanzania wanaelewa mifumo ya uongozi? Kama hawaelewi huko shuleni wanajifunza Nini? Kila Jambo hata Mambo madogo ya kifamilia utasikia MTU anamlilia Rais...
Kwa sababu za fikra za uchawa, chawa hawawezi kuishi bila host.
Rais ndiye host mzuri kuliko wote.
 
Katika nchi ambayo mihimili mingine imeingiliwa na ule ulio chini ya Rais, anaachaje lulaumiwa.?

Wewe ulishaona zuri lolote nchi hii likapita bila Rais kupongezwa? Kwanini ushangae wanapomlaumu kwa mabaya.?
 
Yeye ndio kachagua waku msaidia.
Wakifanya makosa lawama zina mstahiki yeye. Hana pa kukwepea
 
Rais mwenyewe ndio anapenda hivyo, kwani hicho ndio kipimo halisi cha kujua watu wamelala kwa kiasi gani.
Mwambie ukweli huyu pimbi hajielewi kabisa! Tanzania ndio maraisi wamejijengea, badala ya kujenga mifumo, ni misifa TU! Hivi Marekani unaweza kusikia mtu anataka Biden amsaidie kutatua shida yoyote? Shithole countries! Rubbish!
 
Back
Top Bottom