Ni kwanini Lake Victoria,Nyasa na Tanzganyika hazina Fast Ferries

Ni kwanini Lake Victoria,Nyasa na Tanzganyika hazina Fast Ferries

Habari Wanajamvi,
Kuna swali najiuliza kwa muda sana.
Ni kwanini watanzania awajawaza ku-invest kwenye fast ferries(kama zile za Azam) kwenye maziwa yetu?
Iko wazi meli zipo lakini huduma ni za kusuasua sana.
Kwa bahati nzuri tuna ship builder mmoja--Songoro marine na ana yard karibu na hizi maeneo--ni nini kinazuia private companies kufanya operations zinazoeleweka kwenye maziwa haya?
Nimeona waganda wana kampuni ya Earthwise na tayari wameshajiongeza na Welcome To Earthwise Ferries Uganda | Tanzania kuja mwanza---kwanini tumelala?Tunafeli wapi?
Kwanini tuhangaike kujenga mimeli mikubwa wakati hata vidogo vinatushinda?
NA ni kwanini meli nyingi kwenye haya maziwa zinatembeaga usiku tu?-ni swala la kusalama au?
Hao wanaoishi huko nauli ya 2000 ni kubwa kwao...wamezoea kupanda feri wabebe na mizigo yao
 
Magufuli ndio alileta zengwe hizi boat zikazuiwa maana alikuwa na ubia na akina Songoro Marine pamoja na Salma Investment pamoja na wadau wengine kama MV Serengeti.

Aliwapiga Vita hao wahindi wakaona isiwe shida wakampeleka Mombasa. Jamaa alikuwa na roho mbaya ever since.
Hata kwenye ndege.. Aliwaondoa fast jet akifikiri Air Tanzania itakuwa vizuri..
Hakupenda ushindani kabisa.. Aliweka zaidi ya Bil 300 kurekebisha reli ya kaskazini ni jambo jema lakini hakukuwa na mpango wa kushirikisha wafanyabiashara na wenye viwanda.. Lengo lake moyoni lilikuwa kuwayumbisha watu wa Malori...Reli ipo lakini haitumiki
 
Back
Top Bottom