Ni kwanini Manzese miaka ya zamani palikuwa panaitwa Soweto kabla ya Manzese

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,217
Reaction score
3,694
Katika pitapita zangu nilikutana
Taarifa kumbe miaka ya nyuma
Mji wa manzese ulikuwa unaitwa
SOWETO.

KWA WALE WENYE KUMBUKUMBU HEBU MTUAMBIE ILIKUWA HUU
MJI ULIKUWA UNAITWA SOWETO
BADAE SERIKALI UKAITWA MANZESE.

KWA WALE WANA DAR WA KITAMBO HEBU MTUAMBIE ILIKUWAJE
 
Me huwa najua Soweto ni maeneo ya wanaoishi watu jua kali.Kama ilivyo S.Africa,Kil,Chg..
 
Basi miaka manzese palikuwa
Panaitwa soweto hebu tusubili
Wenye mji watuambie
Palikuwa navulugu nyingi saana watu walikuwa wanakunywa pombe masaa24 kukabwa na uporaji vilikuwa vitu vya kawaida wanawake walikuwa wanabakwa ovyo yaani ulikuwa vulumai tupu
 
Duu aiseee kumbe palitisha
Sana namna hiyoo
 
Nilikuwa sijui kama palikuwa panaitwa soweto.
 
Katika pitapita zangu nilikutana
Taarifa kumbe miaka ya nyuma
Mji wa manzese ulikuwa unaitwa
SOWETO.

KWA WALE WENYE KUMBUKUMBU HEBU MTUAMBIE ILIKUWA HUU
MJI ULIKUWA UNAITWA SOWETO
BADAE SERIKALI UKAITWA MANZESE.

KWA WALE WANA DAR WA KITAMBO HEBU MTUAMBIE ILIKUWAJE
unawakumbuka mgambo?basi miaka hiyo nadhanimwishoni mwa 70 au mwanzo mwa 80 hao mgambo walikuwa ndio kila kitu vile polisi wetu wanafanya sasa walikuwa wapelelezi waendesha mashataka na mahakimu.
kisa kilianzia msako wa pombe za kienyeji wakamkamata mama muuza pombe (kulikywa na njaa enzi hizo marufukua nafaka kufanyia pombe) basi kuna mlevi akaripuka ikaanza vurugu mgambo akafyatua ikampata mtoto mdogo wa shule wa kama 10 yrs hivi akafa hapo hapo.
hapo ndio zogo likaanza wale mgambo walikuwa wanapewa shot gun zile za risasi nadhani tamo tu watu wakaanza kumfuata wamwage damu majority wakiwa walevi jamaa akapiga hewani risasi kadhaa watu wakaongezeka (kumbuka mgambo kipindi hicho walikuwa waonevu mno) wakiwa na hasira wakirusha mawe mgamboa akaanza mbio kaishiwa risasihata hivyo watu wakawa confused hawamjuu magambo yupi na wale askari na mgambo waliokuwa maeneo ya karivu walisogea kwenye tukio nao wakashabuliwa ikawa popote ukimkuta mgambo au polisi ni kung'uta mpaka atoke roho mchezo uliisha siku yatatu yake nadgani halafu kitongoji chote cha manzese tandale mburahati midizini mabibo mpaka sinza kukawa chini ya ulinzi kama mwezi hivi .
hivyo ndivyo nakumbuka hadithi ilivyokuwa kupitia kwa wazee wakisimulua mikasa ya vyombo vya usalama
 
Umeieleza vizuri, wakati ule polisi au Mgambo ukileta tabia kama hizi wafanyavyo sasa basi utaijua reaction ya wananchi. Sio leo polisi wanapiga risasi mwanafunzi huko Mikumi watu wanaishia wao na mbunge wao kulia hadharani kijiji kizima! Thubutu wakati ule kingewaka, uonevu wa kijinga ulikuwa hauvumiliki. Hizi tabia kwa mfano wakati wa uchaguzi wa madiwani majuzi hakika roho za askari wengi tuu zingewatoka na sio woga na kukubali kuonewa huku kunakofanyika sasa.
Ila raia nao walikuwa wanaheshimu viongozi na askari wanaofuata maadili yao ya kazi. Viongozi kama Dr Kleruu hawakuwa wanavumiliwa na raia
 
Sasa nini kimetokea watu wamekuwa kama kondoo? Watu wanapigwa na askari bila hatia, wanajeruhiwa na hata kuuliwa lakini hakuna reaction ya wananchi. Angalia kule Ukonga walivyotembeza mikong'oto kwa siku 3 nzima bila raia kufanya lolote. Askari wanafanya watakavyo hata kinyume cha sheria. Lakini mimi naona hawa askari wetu wamebweteka na upole wa wananchi wanachezea pili pili kabla haijapasuka wasiwafanye raia kama mpira wa kupiga watakavyo. Angalia wakati mwingine wanawaweka watu chini ya ulinzi na watu wanatii lakini bado wataendelea kuwapiga marungu na kuwakanyaga kama wanyama wanapopanda na kushuka kwenye magari yao. Mbaya sana!
 
Kuna ujinga umepandikizwa na chama tawala. Bila kukikataa Kuna siku watu wake zao watabakwa na askari na wao wataishia kusema "tunamwachia Mungu"
 
Back
Top Bottom