Ni kwanini Sera na mikakati ya awamu ya tano inapingwa na Wasomi?

Ni kwanini Sera na mikakati ya awamu ya tano inapingwa na Wasomi?

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Unajuwa kuna wakati watu wenye akili lazima tujiulize na kujijibu maswali magumu ambayo hakuna Mtu anakuja hapa kujibu wengi wanasifia na kutetea mambo uwenda mwisho wake hawaujuwi.

Jambo la Kwanza nilazima washauri wa Sera na mipango ya chama na serikali mfike mahali mkumbuke uchumi hauna miujiza wala maombi ila uchumi wa Leo unaongozwa na taratibu mbili tu katika solo Yani demand and supply. Hii hazidanganyi.

Ukizuwia mzunguko wa pesa ktk nchi maana yake unaenda kushusha bei ya bidhaa while watu wako wanakuwa na ukata mkali mwisho unauwa purchasing power PP Jambo linaenda kufanya watu wafunge bihashara nahili sote tumeliona.

Pili serikali inapojikita katika kujenga miradi mikubwa kama SGR, midege, vinu vya kuzalisha umeme hapo unaenda kukomba hazina yote ya Taifa + mikopo Jambo linaenda kufanya serikali kushindwa panga bajeti nyingine kama kuajiri, kupandisha madaraja, manunuzi ya dawa muhim, na kupandisha thaman ya USD why Una nunua Zaid nje kuliko unavyo uza tunasema kunakubwa na unequal balance of payment BOP.

Tatu katika project yeyote kuna kitu tuna same return to investment hii no hesabu inayotumika ku calculate muda mradi utarudisha pesa umewekeza sina uhakika na sidhani kama ktk miradi yote hii mikubwa kuna mahali ambapo serikali imetuambia return itakuwa lini na uwenda ndio maana hii mikataba uwenda haipo wazi kivile. Nahapa kama mtakuwa mnakumbuka baada ya mauza uza ya Lowassa na rich mond kukawa na maazimio Kuwa serikali isiingie mkataba bila kwenda bungeni sina uhakika kama mikataba hii ya ma Trillion kama serikal ilipeleka bungeni wakaipitia sijuwi walimtumia vifungu gani ila nadhan hii inawapa nguvu wapinzan kuongea.

Nne kutokana na hayo nimeya andika Kwa ufupi ndio Siri ya Kwa nn mapingamizi nimakali Kwa serikali ya awamu ya tano.
Jambo linapigiwa kelele nikuwa hii miradi isije Kuwa white elephant kutokana na usiri.
 
TumainEl -- Are you a development Economist ?

This is more of an Intellectual debate and not as simple discussion as you want it to appear.

Public investment by Tanzania Government and local governments builds the nation’s capital stock by devoting resources to the basic physical infrastructure (such as roads, bridges, rail lines, airports, and water distribution), innovative activity (basic research), green investments clean power sources (hydro power) and education (both primary and advanced, as well as job training) that leads to higher productivity and/or higher living standards.

While private actors also invest in these areas, they do so to a much smaller degree, in part because the gains from public investment accrue not just to those undertaking the investment, but to a wide range of people and businesses.

In recent years, some debate has centered around increasing public investment to provide a near-term boost to the job market, based on research showing that infrastructure investment is about the most efficient fiscal support one can provide to a depressed economy.

But there is also an enormous amount of economic evidence demonstrating that public investment is a significant long-run driver of productivity growth—and hence growth in average living standards.

This lesson was lost in recent decades because —in a break from historical trends—productivity acceleration in the late 1990s was driven largely by private-sector investments in information and communications technology (ICT) equipment, and not by increased public investments.
 
Tatizo ni sera za majukwani ambazo hazina sheria na kanuni za kuzisimamia kwa awamu hii niza mtu mmoja 'uncertainty policy ' pia ukosefu wa elimu ya ujasiriamali kwa viongozi wakitaifa 'in entrepreneurship we learn how to do business not about business '
 
Mtaji wa CCM ni ujinga wa Watanzania
Sio kweli. Ma shabiki wengi wa saccos ya ufipa ni vipofu wa fikra. Hivyo kipofu akimwongoza kipofu wote hutumbukia shimoni, ndicho Lissu na genge lake wanang'ang'ana kuvuta watanzania.

Rais Magufuli na Serikali yake, wamejipambanua kwamba ni Serikali ya viwanda so akaamua kuonyesha njia kwa kutangulia mbele kwa vitendo leo hii ametufikisha uchumi wa kati. Tanzania mpya inakuja.
 
Wasomi gani hao, maana kuwa na cheti haimaanishi una akili
 
Sio kweli. Ma shabiki wengi wa saccos ya ufipa ni vipofu wa fikra. Hivyo kipofu akimwongoza kipofu wote hutumbukia shimoni, ndicho Lissu na genge lake wanang'ang'ana kuvuta watanzania.Rais Magufuli na Serikali yake, wamejipambanua kwamba ni Serikali ya viwanda so akaamua kuonyesha njia kwa kutangulia mbele kwa vitendo leo hii ametufikisha uchumi wa kati. Tanzania mpya inakuja.
Haa hivi hujui km mabeberu wametushusha kwenye uchumi wa kati
 
SGR na midege ni white elephants, wakubisha na wabishe lakini muda utaongea,

Ikiwa reli ya TAZARA inayokwenda upande ambako asilimia kubwa ya mizigo inayopita bandarini dsm inakwenda imedoda unadhani nini kitakua cha tofauti kwenye SGR?
 
This lesson was lost in recent decades because —in a break from historical trends—productivity acceleration in the late 1990s was driven largely by private-sector investments in information and communications technology (ICT) equipment, and not by increased public investments.
Can you clarify more on this.... What's wrong with private-sector-driven investments?
 
TumainEl -- Are you a development Economist ?

This is more of an Intellectual debate and not as simple discussion as you want it to appear...

Ambiere Maghembe sikuona haja yoyote ya kucopy paragraph za kiuchumi na kuja kuzipaste hapa. Hii inaonyesha unatambia ubora wa elimu ya kukariri. Na dalili zote zinaonesha ww ni limbukeni wa kiingereza, ndiyo maana unadhani ukiweka maelezo ya kukariri ya kiingereza utakuwa na ubora wa hoja. Mleta hoja kaja na mada ya ugumu wa maisha ya wananchi, ungekuja na maelezo marahisi kwanini ugumu huu wa maisha, je hakukuwa na njia mbadala wa hali hii? Badala yake umekuja na maelezo ya kiingereza yasiyojibu hoja zake kwa ufasaha zaidi ya blablaa za kiingereza.

Sasa twende pamoja ili ujue huna msaada wowote. Wakati wa JK tuliimbishwa umeme wa gas sijui uchumi wa gas whatever you may call it. Tuliambiwa bomba la gas likifika Dar tatizo la nishati itakuwa historia! Wakati huo huyu mwenye mradi wa umeme wa maji alikuwa waziri, huku akiwa kimya kwenye pambio hilo. Mradi ule tuliambiwa ukikamilika utazalisha umeme wa 5,000mg. Tukakopa 1.5t or so, I stand to be corrected. Kufanya mradi ule, ambao una phase tofauti tofauti kama kinyerezi I, II nk. Mahitaji ya umeme hapa nchini hayazidi 2,000mg, na kwa sasa tuna 1,500m+. Kwanini rais aumize nchi kwa kukopa au kutoa huko anakojua kufanya mradi wa 6.5t wa maji, badala ya kuweka wangalau 2t kuongeza umeme wa gas, ambao hadithi za mwanzo ilikuwa tutapata 5,000mg v/s 2115mg wa hydro?

Mradi wa SGR, mradi huu wakati wa JK alikuwa amekamilisha kila kitu, na wakakubaliana mradi huu ujengwe kwa $7b (14t Tshs) mkopo wa Exim bank ya China, Kisha malipano yatafanyika wakati mradi unafanya kazi. Ila sharti namba moja la huo mkopo ilikuwa ni lazima mkandarasi awe mchina. Alipoingia Magufuli akabadili mkataba na mkandarasi kwa maelezo kuwa kuna cha juu (over estimate) kwenye mkataba wa JK. Yeye alisema atajenga mradi huo kwa 7.5t Tshs, na mkandarasi sasa ni mturuki. Lakini kuna tetesi zinazoonyesha gharama zitarudi zile zile estimate za mwanzo za JK, not sure of this, lakini kwa vyovyote utavuka 10t.

Lakini lililo dhahiri ni kuwa mpaka sasa timeshakopa 3.1t kwenye huo mradi, huku terms za mkopo zikiwa kificho kabisa. Kilio chetu ni kwanini watu wengine waumie kwa miradi ya kusaka sifa za mtawala, huku yeye na kundi lake sio sehemu ya maumivu yetu, maana huduma zote wanapata bure? Ifahamike hapa hatupingi, bali tunasema kulikuwa na njia nyingine nzuri za kutekeleza haya mambo bila kuumiza watu kwa kiwango hiki. Siku hizi mkiishiwa hoja huwa mnajificha kwenye kichaka cha kupinga kila kitu. We need proper explanation in Swahili not in English in these key areas, as your English is not good, and your Swahili is not even better.
 
Mkuu Tuma, nikwambie kitu kimoja ambacho kama vile unajisahaulisha au kujifanya hujui wakati unajua kabisa kuwa hakuna mkataba wowote wa manunuzi ya ndege, wala makubaliano ya ujengaji uwanja wa Chato kwa hiyo kampuni tajwa wala ujengaji wa SGR na waturuki iliyowahi kujadiliwa bungeni.

Kwanini tusiite elaphant project kwa mfano mpaka sasa hatujui TTCL ina run on profit or loss? Kwanini CAG hawezi kuikagua?
Kwanini tusiite elephat project kwakujenga International airport kijijini wakati airstrip tu ingetosha kule Chato; what's the economic implication and benefit to build such airport there?

Kwanini tusiwe na mashaka kama miaka mitano tu tumekamilisha kipande cha Dar to Moro SGR je miaka mitano mingine ataweza kukamilisha Moro to Kigoma?

Sikuona haja ya kuanzisha miradi mikubwa mingi wakati tungeweza kufanya mmoja mmoja na kubalance money circulation. Kurupukurupu yote hii ili apige hela na wenzake chini ya mgongo wa miradi.
 
Can you clarify more on this.... What's wrong with private-sector-driven investments?
This is a bit complex, we need time and good exchanges for you to grasp in full what public / private investments is all about.

I am a member of Consultants and advisors of World Bank Group, connect with me at IBRD (World Bank) / Africa Develepment Bank Group./ LinkedIn, we will talk more.

Both the public and private sector have a role to play. For general businesses without externalities, the private sector is likely to be more efficient and better at job creation. Reducing the scope of government spending could create more private sector opportunities for investment and job creation.

However, the private sector also needs a good public sector to provide, education, healthcare and infrastructure investment. Also, the private sector needs a stable macro-economy which the government has a role to provide. In a prolonged recession, the case for government intervention to create jobs is much stronger than when the economy is growing strongly.
 
Ukiwa kiongozi, hata ufanye maendeleo kiasi gani, kuna watu watakupinga tu. Yako wapi ya Gaddafi na Libya??!
.
Huwezi kuwa kiongozi ukamfurahisha kila mtu, its just impossible.
 
Ambiere Maghembe sikuona haja yoyote ya kucopy paragraph za kiuchumi na kuja kuzipaste hapa. Hii inaonyesha unatambia ubora wa elimu ya kukariri. Na dalili zote zinaonesha ww ni limbukeni wa kiingereza, ndiyo maana unadhani ukiweka maelezo ya kukariri ya kiingereza utakuwa na ubora wa hoja. Mleta hoja kaja na mada ya ugumu wa maisha ya wananchi, ungekuja na maelezo marahisi kwanini ugumu huu wa maisha, je hakukuwa na njia mbadala wa hali hii? Badala yake umekuja na maelezo ya kiingereza yasiyojibu hoja zake kwa ufasaha zaidi ya blablaa za kiingereza....

Nilicho fanya kwanza kinacho jadiliwa kiwe wazi, kwa kuwa ameandika kwa ufupi, baada ya hapo tuende kidogo kidogo na tufike sehemu yeye ataelewa na mimi nitajua malalamike yake.

Hili ni eneo mimi nipo Alhamdulilah, nafikiri nina uwezo nalo tuu sana. Hata wewe mbishi mbishi utafaidika.

Tujifunze kujaribu kuelimishana na sio kushindana, hili sio jukwa la kushindana ni kuelimishana. Na ndio ubora wa JF ila watu kama ninyi mnataka kuuharibu.
 
.
Ukiwa kiongozi, hata ufanye maendeleo kiasi gani, kuna watu watakupinga tu. Yako wapi ya Gaddafi na Libya??!
.
Huwezi kuwa kiongozi ukamfurahisha kila mtu, its just impossible.
Hufuati sheria kwa wakulima,wafanyabiasha, wafanyakazi, wasomi wanahitaji kazi basi tengeneza mazingira yawe rahisi kwao wewe ndio unawadidimiza kwa matakwa binafsi, na Gaddafi aliondolewa kwa chuki na wivu wa nchi za magharibi, maana hata kama alikuwa na mabaya gani lakini wananchi walipewa dola 400 kwa kila mtu ambaye hana ajira, njoo bongo sasa tunarasilimali za kutosha, basi zitumike vizuri ili kumsaidia mwananchi wa kawaida, mmebaki na mapambio yenu miaka 59 hatuna dira kama nchi na hatujui tufanye nini kwa future generations
 
Back
Top Bottom