Ni kwanini Sera na mikakati ya awamu ya tano inapingwa na Wasomi?

Ni kwanini Sera na mikakati ya awamu ya tano inapingwa na Wasomi?

Nilicho fanya kwanza kinacho jadiliwa kiwe wazi, kwa kuwa ameandika kwa ufupi, baada ya hapo tuende kidogo kidogo na tufike sehemu yeye ataelewa na mimi nitajua malalamike yake.

Hili ni eneo mimi nipo Alhamdulilah, nafikiri nina uwezo nalo tuu sana. Hata wewe mbishi mbishi utafaidika.

Tujifunze kujaribu kuelimishana na sio kushindana, hili sio jukwa la kushindana ni kuelimishana. Na ndio ubora wa JF ila watu kama ninyi mnataka kuuharibu.

Hatuhitaji kiingereza chako maana sio kizuri, ongea hoja kwa kiswahili tena fasaha, ili kila mtu aone unachoongea na kupima ubora au usahihi wa hoja zako. Halafu ww sio SI Unit wa michango bora ya hoja za hapa jukwaani. Anayetaka kuharibu jukwaa kuna sheria anapewa ban, wala hilo sio jukumu lako. Ukiona mchango wowote unaotezwa utu wa member yoyote, kuna kitufe(report button) cha kutoa taarifa ya ukiukwaji wa sheria za jukwaa. Hoja nyingine zozote ni halali, hivyo utapaswa upambane na hali yako. Sasa jikite kwenye post namba moja, kwanini hali za wananchi zimekuwa ngumu kwa kiwango hiki?
 
.
Ukiwa kiongozi, hata ufanye maendeleo kiasi gani, kuna watu watakupinga tu. Yako wapi ya Gaddafi na Libya??!
.
Huwezi kuwa kiongozi ukamfurahisha kila mtu, its just impossible.

Usitake kupotosha kuhusu kufurahishwa na kupata stahiki zako. Wafanyakazi wanapaswa kupandishwa mishahara kwa mujibu wa sheria, na wala sio suala la kufurahishana. Watu wanahitaji ajira, ni mwaka wa tano sasa ajira imekuwa tatizo.

Wakati huo huo sekta binafsi zinazidi kufunga shughuli zake, kutokana na changamoto mbalimbali na nyingi ya changamoto hizo, ni serikali kutumia mbinu ya kukomoa zaidi, kuliko kujenga njia rafiki za kusonga mbele. Jitahidi kutokuchanganya kufuruhishana na wajibu.
 
Ambiere Maghembe sikuona haja yoyote ya kucopy paragraph za kiuchumi na kuja kuzipaste hapa. Hii inaonyesha unatambia ubora wa elimu ya kukariri. Na dalili zote zinaonesha ww ni limbukeni wa kiingereza, ndiyo maana unadhani ukiweka maelezo ya kukariri ya kiingereza utakuwa na ubora wa hoja. Mleta hoja kaja na mada ya ugumu wa maisha ya wananchi, ungekuja na maelezo marahisi kwanini ugumu huu wa maisha, je hakukuwa na njia mbadala wa hali hii? Badala yake umekuja na maelezo ya kiingereza yasiyojibu hoja zake kwa ufasaha zaidi ya blablaa za kiingereza...

1)Nina uwezo mzuri kabisa wa kujibu, lakini wewe unataka niwajibie maswali yako wako walioamua hiyo miradi. Mimi nitajibu tuu nionavyo mimi na sitaki niwajibie.

2) Kwa mimi nafikiri na ni kipima na wenzangu ambao kiingereza ni lugha ya kwanza naamini ni muandishi mzuri tuu hasa kiingereza na professional issues kiingereza ni lugha rahisi kwangu. Kwa kishwahili naweza kuandika kuwasiliana na kwa ubora na nikaeleweka.

3) Kwa uwezo wa kichwa chako kufuatana na michango yako ningefurahi nikakujibu kwa swali moja moja na kwa maelezo ya kukutosha.

Muda huu ni 11.33 PM tuulaze mjadala huu kesho nikipata muda utapata madini ya kukutosha. Asante.
 
Sasa jikite kwenye post namba moja, kwanini hali za wananchi zimekuwa ngumu kwa kiwango hiki?

Bila kuonesha jazba na kusifia ili wengine waonekane wapingaji tu. Swali hili huwa halijibiwi
 
1)Nina uwezo mzuri kabisa wa kujibu, lakini wewe unataka niwajibie maswali yako wako walioamua hiyo miradi. Mimi nitajibu tuu nionavyo mimi na sitaki niwajibie...

Sitaki nikupeleke kwenye kona ngumu, ngoja nisubiri majibu yako. Japo kama utakuwa hujibu kinacholeta hali hii, sijui utakuwa unajibu nini! Eagerly waiting for your lovely stories.
 
Kwa sababu binadamu wanataka waamue maendeleo yao wenyewe na wanataka waweke vipaumbele vyao wenyewe kwa ujumla na sio mtu mmoja.
.
Ukiwa kiongozi, hata ufanye maendeleo kiasi gani, kuna watu watakupinga tu. Yako wapi ya Gaddafi na Libya??!
.
Huwezi kuwa kiongozi ukamfurahisha kila mtu, its just impossible.
 
.
Ukiwa kiongozi, hata ufanye maendeleo kiasi gani, kuna watu watakupinga tu. Yako wapi ya Gaddafi na Libya??!
.
Huwezi kuwa kiongozi ukamfurahisha kila mtu, its just impossible.
Wajinga wengi huwa wanaongea kama wewe maendeleo yasiyojali return
 
Nilicho fanya kwanza kinacho jadiliwa kiwe wazi, kwa kuwa ameandika kwa ufupi, baada ya hapo tuende kidogo kidogo na tufike sehemu yeye ataelewa na mimi nitajua malalamike yake.

Hili ni eneo mimi nipo Alhamdulilah, nafikiri nina uwezo nalo tuu sana. Hata wewe mbishi mbishi utafaidika.

Tujifunze kujaribu kuelimishana na sio kushindana, hili sio jukwa la kushindana ni kuelimishana. Na ndio ubora wa JF ila watu kama ninyi mnataka kuuharibu.
Mpaka hapa bado hujaelimisha kitu
 
Sio kweli. Ma shabiki wengi wa saccos ya ufipa ni vipofu wa fikra. Hivyo kipofu akimwongoza kipofu wote hutumbukia shimoni, ndicho Lissu na genge lake wanang'ang'ana kuvuta watanzania.Rais Magufuli na Serikali yake, wamejipambanua kwamba ni Serikali ya viwanda so akaamua kuonyesha njia kwa kutangulia mbele kwa vitendo leo hii ametufikisha uchumi wa kati. Tanzania mpya inakuja.
Serikali ya viwanda , viwanda vipi ivyo.
 
Back
Top Bottom