Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumekuwa tukiwasikia sana watetezi wa utawala huu wa awamu ya tano wakitetea sana uminyaji wa demokrasia unaofanywa na serikali hiyo kuwa ni sahihi kwa madai ya kutumia kivuli cha kuleta maendeleo ya nchi hii.
Mifano mikubwa wanayotoa hao watetezi wao ni kasi ya maendeleo wanayodai inafanywa na watawala wa serikali hii, kama vile ujenzi wa reli ya SGR, ujenzi wa bwawa la umeme la Stiegler's Gorge na ununuzi wa ndege za Bombardier unaofanywa na serikali hii.
Nipende kuwauliza hao watetezi wa awamu hii kuwa hivi kama kweli wanaamini kuwa serikali hii inawafanyia maendekeo makubwa wananchi wake, ambapo hakuna mwananchi asiyeyaona, si wangeacha wananchi wenyewe waamue kuchagua viongozi wao wanaowataka kupitia sanduku la kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki?
Mfano halisi ni namna serkaki hii ya awamu ya tano kwa namna ilivyouviruga uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, ambapo vyama 8, kikiwemo chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema kulazimika kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.
Kama wanachoongea ni kweli kuwa hata kipofu anayaona maendeleo yanayofanywa na serikali hii ya awamu ya tano, iweje sasa serikali hii hii iogope kupita kiasi kufanya chaguzi zilizo huru na haki?
Hivi ni kwanini hawawachi wananchi wenyewe ndiyo wachambue mchele na pumba?
Ni kwanini basi watawala ndiyo wanaowachagulia wananchi viongozi wao wanaowawakilisha?
Hivi tukiangalia kwenye nchi za wenzetu zilizoemdelea kama vile Taifa kubwa kiuchumi duniani la Marekani, ni kwanini wao hawaminyi demokrasia na badala yake wanahimiza izidi kupanuliwa?
Na hizi propaganda zao hawa CCM kuwa Maendeleo hayawezi kuja nchini kwa kuimarisha demokrasia ni mawazo potofu sana.
Huu mfumo waliouchàgua hawa CCM wa kurejea kwa nguvu kwa mfumo wa chama kimoja ni mfumo wa kidekteta na ambao utatuletea machafuko nchini kwetu na ni mfumo unaovunja kwa makusudi mfumo ulioanishwa ndani ya Katiba ya Jamburi ya muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo nainukuu "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafuata mfumo wa kidemokrasia na ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.
Nakaribisha maoni yenye maslahi mapana na itakayoonyesha dira ya mustakabali mwema wa taifa letu.