Ungejiuliza kwanini walienda Somalia? Utapata jibuJapo sifahamu kiundani zaidi lakini mambo haya yameanzia wapi lakini taifa la kenya limekuwa likishambuliwa na wana kikundi cha al shababu kwa miaka kadhaa
na hawa al shababu wanadai chanzo cha kuishambulia kenya ni kwa sababu wamepeleka majeshi yao nchini somalia katika ngome ya al shababu sasa kama ndo hivyoo
ni kwanini serikali ya kenya isiondoe jeshi lake nchini somalia ili raia wake waishi kwa amani tuuu ?????
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndio ukweli! Kenya wajitoe kwenye mapigano yasio na faida kwao.
Kila mtu na mtazamo wake! Kenya ndio adui alievamia ardhi ya Somalia, nadhani akiondoa jeshi lake Somalia hii vita itakua imekwisha.Je kwenye janga la moto "fire break" husaidiaje? au ipi bora upigane na adui ndani ya nyumba yako au upigane naye akiwa kwake?
Kenya waliingia Somalia kwenda kuzuia utekaji watu mpakani uliokuwa unafanywa na Alshabaab. Tunakumbuka hata Ethiopia nao waliwahi kuingia Somalia kupambana na Alshabaab, walipoona hakuna faida wakaondoka.
Tatizo ni kuwa Alshabaab hawana jeshi moja lililopo kwenye kambi zilizo rasmi, bali wana mtandao wa cells. Cells zinaweza kuwasiliana, kusafirisha silaha, kushambulia na kupata mafunzo mahali popote. Tofauti na majeshi yanayojua uniform, kambi, magari ya jeshi, na zana rasmi za kupigania.
Lazima Kenya wawekeze kwenye mafunzo yatakayoweza kukabiliana na mfumo wa mapambano wa Alshabaab. Mfumo wa jeshi na polisi wa kawaida hauwezi kupambana na Alshabaab.
Tatizo lingine ni kukosekana umoja kwa waafrika katika kukabiliana na changamoto kubwa kubwa. Mimi sioni sababu ya kila ka-nchi kujiendea inavyoona yenyewe. Ni lazima baadhi ya mamlaka yachukuliwe na jumuiya kubwa zaidi mfano kuunda jeshi moja la EAC. Jeshi hili linaweza kupewa mandate ya kupambana na wakorofi wote na hata wale wanaong'ang'ania madarakani na kusababisha vita za wenyewe kwa wenyewe.

Bora kwake maana kwako ni hasaraJe kwenye janga la moto "fire break" husaidiaje? au ipi bora upigane na adui ndani ya nyumba yako au upigane naye akiwa kwake?
Kwa nn MzeeeSema hapo unaposema EAC wafanye mambo kwa pamoja ndo unakosea. Hawa kweli ni ndugu zetu na tunashirikiana sana ila hili l la Al shabab aisee hapana
Sent using Jamii Forums mobile app
KIONGOZI UNACHOKIZUNGUMZA SI KWELI KWAMBA KENYA NDO IMEPAKANA NA SOMALIA PEKEE HAPANA .......Mkuu tambua kuwa Jeshi la kenya liliingia Somalia kwa mwamvuli wa AMISOM (AU), ninachokiona ni kwamba Kenya imekuwa targeted sana Kwa sababu:-
1.Ndiyo nchi iliyopo karibu na Somali kati ya nchi zenye majeshi huko mfano Uganda, Burundi, Ethiopia n.k.
2. Kenya na Alshabab wana historia ya vita tangu kipindi cha nyuma, mfano kipindi cha uharamia katika eneo la bahari la Kenya, wahusika walikuwa hao hao Alshababu.
Cha kufanya,
Kenya isiondoe jeshi lake Somalia, ila wawekeze zaidi kwenye mbinu za kiupelelezi na ikiwezekana wasitoe au kusikiliza maelekezo ya wazungu kuhusu namna ya kukabiliana na ugaidi kwa sababu hao ndio wawezeshaji wa ugaidi.
Pia waimarishe zaidi vikosi vya uokoaji hasa kwenye vikosi vyo "Komandoo" na polisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi hawaelewi kwamba hawa magaidi ni vichaa wa kutupwa. Ila ukiangalia maoni ya wengi wa hawa watani wetu utagundua kwamba walitizama zile video za yale mahubiri ya Makaburi na Aboud Rogo, na wakaamini propaganda zao. Leo hii alshabaab wamehamia kwenye Trump na uamuzi wake kuhusu Jerusalem. Kabla ya KDF kuingia Somalia ilikuwa ni Israel na 'blockade' yao kule Gaza. Kesho KDF wakiamua kutoka Somalia wataendeleza mashambulizi ukanda huu kwa kisingizio cha uvamizi wa vikosi vya kigeni kule Syria.Alshabaab wametoa tamko kwamba walifanya walichokifanya kwa sababu Trump ameitambua Jerusalem, unafaa kufahamu gaidi huhamisha goli maana neno 'amani' ni hasara kwake.
Shida nini?Kwa nini mods wasifute nyuzi zingine za kishenzi?
Shida ni pale binadamu mwenzio anakucheka ukikabiliwa na janga na kusema mauti yanakufaa kwa sababu ya maumbile!!Shida nini?