Ni kwanini uhai wa mapenzi ya kujionyesha mbele za watu kwamba mnapendana sana huwa hayadumu?

Ni kwanini uhai wa mapenzi ya kujionyesha mbele za watu kwamba mnapendana sana huwa hayadumu?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Mifano ni mingi sana humu nchini.

Hivi shida hasa huwa ni nini, licha ya kujiapiza na kusifiana kupitiliza mtaani, mitandaoni na kwenye vyombo vya habari mpaka kutoa machozi, lakini mwisho wa siku ndoa au uhusiano una sambaratika vizuri tu.

Huwa ni macho ya watu wabaya au maombi mabaya ya watu yanafanya kazi? Maana kuna wengine ukiwaona tu jinsi wanavyosifiana, hadi unasema wamezaliwa pamoja.

Lakini maadui na wajuvi wa kusoma mambo ya mahusiano huwahesabia siku, wiki na miezi tu wachumba wanatifuana dah!

Kumbe ni afadhalli kuinjoy kimyakimya na likibuma linabuma kimyakimya right?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwa sababu mmoja kati yenu alikuwa anamuonyesha mpenzi kuwa naye anaweza kupendwa.
Ila kuna watu wazima huwa wanawaonea huruma wapenzi vijana wa dizaini hiyo, ila wanashindwa kuwaambia tu...🐒
 
Me naona haijalishi yako public au uchochoroni rate ya kuvunjika ni ile ile, utofauti ni kua haya ya privacy/uchochoroni hatutajua mkiachana hivyo no body count.
 
Back
Top Bottom