Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?



Hospitali ni maalum kwa ajili ya Usalama na watu wa category ya uangalizi wao kama viongozi; maafisa usalama na familia zao

Kwenye Usalama kila kitu ni SIRI hivyo kuugua ni jambo la faragha hata ingekua Muhimbili ila ikiwa amekufa SIO siri Tena
 
Kwa hiyo Rais kama anaumwa mahututi hata hana fahamu, wananchi hawana haki ya kujua hilo?

Kama unataka faragha zako, usigombee uongozi.

Ukigombea uongozi, umekubali kujiondolea faragha zako.

Hutakiwi kugombea uongozi, halafu utake kuwa na faragha za watu wasio viongozi.

You can't eat your cake and have it too.
 
Mkuu kuwa kiongozi bado haiondoi haki yake, Kama binadamu, kwani Rais ni Mungu, au roho mtakatifu, kile ni cheo tu maana hata wewe kesho waweza kuwa Rais ila bado wewe ukitoa cheo unabaki wa kawaida, hakuna mahitaji yoyote watakiwa kuwa nayo tofauti na binadamu tofauti ya kwako yatakua high quality, but physiologically nothing more changable, you will digest and your waste product will be get out through specific organ as usual ,ila ugonjwa wa mtu utabaki siri , KWA mhusika mkuu, labda ukiruhusu,au pawepo sababu za msngi
 
Hivi kuna kiongozi hapo Tz akigonjeka thamani ya hisa kwenye soko inashuka?

Kwa kweli sidhani kuwa hao wanaotibiwa humo wana significance yoyote zaidi ya wabongo wengine ukiachilia mbali kwamba watanzania wengi wanapenda kutengeneza askari wanasesere na kisha kuwaangusha.

Au kujenga nyumba za karatasi alafu kuziporomosha!
 

Unakuwa “a goldfish in a glass bowl”.

No hiding place.
 
Taratibu mkuu... Pole kwa kichoshwa na kadhia hii
Zaidi ya Mwanafamilia huyu wa Mzena Rosemary Mzena, unaweza kunitajia Mzena Mwingine aliyepoteza maisha pale Mzena? Karibu
 
Wewe utapenda kuwa na Rais mwenye kifafa anayeanguka anguka kila siku hadharani na kuiweka nchi kwenye mtafaruku, kwa sababu hajasema ana kifafa alivyokuwa anagombea urais?

Unaelewa hiyo unayoita haki yake ya faragha inaweza kumfanya afe, kwa kuwa umeendekeza faragha katika kazi ambazo hazitaki kuendekeza faragha, na umempa kazi yenye stress mtu ambaye hawezi kustahimili stress, na hizo stress zikafanya aanguke na kufa?
 
Unakuwa “a goldfish in a glass bowl”.

No hiding place.
Ndiyo maana watu wengine tunaojielewa na kuthamini faragha zetu tumekataa kugombea uongozi hata wa mtaa.

Tunajua, ukishagombea uongozi tu, unapunguza faragha sana.

Sasa nashangaa watu wanachagua viongozi, halafu bado wanategemea viongozi wawe na faragha.

You can't eat your cake and have it too.

Kama unataka faragha, usigombee uongozi.

Kama unagombea uongozi, usitegemee faragha sana.

It is as simple as that.
 
Kwa kifupi ile hospital ipo chini ya TISSCCM na viongozi waandamizi hata wastaafu pia
 
Leo umeongea ujinga [emoji16][emoji16]....

Nambie lakini mkuu heri ya mwaka mpya
 
Kuna cafeteria kule juu kabisa,labda waihamishe au walishaihamisha maana ni miaka zaidi ya 4 sijapanda kule
Naona Ndugu unazidi tu kuwapa Taarifa juu ya hilo eneo huko juu ili kuanzia sasa Waanze kulifanyia Kazi ama walifunge / wawe wanakaa wao tu.
 
Kwa kifupi ile hospital ipo chini ya TISSCCM na viongozi waandamizi hata wastaafu pia
Asante kwa Kunielimisha zaidi kuhusu hili kwani wengine tuko huko Kisiwani Pemba tunapara zetu tu Samaki na hiyo TISS tulijua ni Hoteli Kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…