Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!

Hospitali ni maalum kwa ajili ya Usalama na watu wa category ya uangalizi wao kama viongozi; maafisa usalama na familia zao

Kwenye Usalama kila kitu ni SIRI hivyo kuugua ni jambo la faragha hata ingekua Muhimbili ila ikiwa amekufa SIO siri Tena
 
Nafikili mtoa mada alimanisha wananchi kupewa tahalifa tu kwamba kiongonzi flani anaumwa kalazwa,hospitali flani basi but aina ya ugonjwa sio lazima kuitoa public bila consert ya mgonjwa, na kweli ugonjwa bado unabaki siri ya mgonjwa na mtoaji huduma wake
Vinginevyo kwa kuzitoa tahalifa bila ruhusa ya mhusika sio tu inakiuka mahadili ya kitabibu bali pia ya mgonjwa husika, labda tu Kama ugonjwa una vihatarishi katika jamii waweza kutoa tahalifa ili jamii kujikinga
Kwa hiyo Rais kama anaumwa mahututi hata hana fahamu, wananchi hawana haki ya kujua hilo?

Kama unataka faragha zako, usigombee uongozi.

Ukigombea uongozi, umekubali kujiondolea faragha zako.

Hutakiwi kugombea uongozi, halafu utake kuwa na faragha za watu wasio viongozi.

You can't eat your cake and have it too.
 
Kwa hiyo rais kama anaumwa mahututi hata hana fahamu, wananchi hawana haki ya kujua hilo?

Kama unataka faragha zako, usigombee uongozi.

Ukigombea uongozi, umekubali kujiondolea faragha zako.

Hutakiwi kugombea uongozi, halafu utake kuwa na faragha za watu wasio viongozi.

You can't eat your cake and have it too.
Mkuu kuwa kiongozi bado haiondoi haki yake, Kama binadamu, kwani Rais ni Mungu, au roho mtakatifu, kile ni cheo tu maana hata wewe kesho waweza kuwa Rais ila bado wewe ukitoa cheo unabaki wa kawaida, hakuna mahitaji yoyote watakiwa kuwa nayo tofauti na binadamu tofauti ya kwako yatakua high quality, but physiologically nothing more changable, you will digest and your waste product will be get out through specific organ as usual ,ila ugonjwa wa mtu utabaki siri , KWA mhusika mkuu, labda ukiruhusu,au pawepo sababu za msngi
 
Hivi kuna kiongozi hapo Tz akigonjeka thamani ya hisa kwenye soko inashuka?

Kwa kweli sidhani kuwa hao wanaotibiwa humo wana significance yoyote zaidi ya wabongo wengine ukiachilia mbali kwamba watanzania wengi wanapenda kutengeneza askari wanasesere na kisha kuwaangusha.

Au kujenga nyumba za karatasi alafu kuziporomosha!
 
Hapana, you have it backwards.

Unavyozidi kupanda kwenye uongozi ndivyo haki yako ya kuwa na faragha inavyozidi kupungua.

Kuna kanuni za maadili ya uongozi zitataka upeleke list ya mali zako ziangaliwe, hapo huna faragha.Kuna kampeni za kuomba kura zitataka uelezee maisha yako yamekuwaje, hapo huna faragha, kuna waandishi wa habari watakuhoji, hapo huna faragha.

Mimi naweza kukaa maisha yangu yote sijapigwa picha na kuwekwa gazetini. Naweza kuilinda faragha yangu hivyo kwa sababu sina uongozi.

Rais wa nchi akikataa picha yake isiwekwe gazetini kwa sababu anataka kulinda faragha yake watu wataona kituko.

Kwa sababu kazi ya urais inaendana na kutokuwa na faragha, mtu anayependa faragha zake anatakiwa ajue kabla hajagombea urais kwamba, kama anataka faragha, asigombee urais.

Ukishagombea uongozi unakuwa "public property", huna faragha tena.

Unakuwa “a goldfish in a glass bowl”.

No hiding place.
 
Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Taratibu mkuu... Pole kwa kichoshwa na kadhia hii
Zaidi ya Mwanafamilia huyu wa Mzena Rosemary Mzena, unaweza kunitajia Mzena Mwingine aliyepoteza maisha pale Mzena? Karibu
 
Mkuu kua kiongozi bado haiondoi haki yake, Kama binadam, kwani rais ni mungu, au roho mtakatifu, kile ni cheo tu,maana hata wewe kesho waweza kua rais,ila bado wewe ukitoa cheo unabaki wa kawaida,hakuna mahitaji yoyote watakiwa kuwa nayo tofauti na binadam tofauti ya kwako yatakua high quality, but physiologically nothing more changable, you will digest and your waste product will be get out through specific organ as usual ,ila ugonjwa wa mtu utabaki siri , KWA mhusika mkuu, labda ukiruhusu,au pawepo sababu za msngi
Wewe utapenda kuwa na Rais mwenye kifafa anayeanguka anguka kila siku hadharani na kuiweka nchi kwenye mtafaruku, kwa sababu hajasema ana kifafa alivyokuwa anagombea urais?

Unaelewa hiyo unayoita haki yake ya faragha inaweza kumfanya afe, kwa kuwa umeendekeza faragha katika kazi ambazo hazitaki kuendekeza faragha, na umempa kazi yenye stress mtu ambaye hawezi kustahimili stress, na hizo stress zikafanya aanguke na kufa?
 
Unakuwa “a goldfish in a glass bowl”.

No hiding place.
Ndiyo maana watu wengine tunaojielewa na kuthamini faragha zetu tumekataa kugombea uongozi hata wa mtaa.

Tunajua, ukishagombea uongozi tu, unapunguza faragha sana.

Sasa nashangaa watu wanachagua viongozi, halafu bado wanategemea viongozi wawe na faragha.

You can't eat your cake and have it too.

Kama unataka faragha, usigombee uongozi.

Kama unagombea uongozi, usitegemee faragha sana.

It is as simple as that.
 
Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Kwa kifupi ile hospital ipo chini ya TISSCCM na viongozi waandamizi hata wastaafu pia
 
Kiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".

Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.

Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".

Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.

Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.

That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.

Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.

Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.

Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?

Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.

Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?
Leo umeongea ujinga [emoji16][emoji16]....

Nambie lakini mkuu heri ya mwaka mpya
 
Kuna cafeteria kule juu kabisa,labda waihamishe au walishaihamisha maana ni miaka zaidi ya 4 sijapanda kule
Naona Ndugu unazidi tu kuwapa Taarifa juu ya hilo eneo huko juu ili kuanzia sasa Waanze kulifanyia Kazi ama walifunge / wawe wanakaa wao tu.
 
Kwa kifupi ile hospital ipo chini ya TISSCCM na viongozi waandamizi hata wastaafu pia
Asante kwa Kunielimisha zaidi kuhusu hili kwani wengine tuko huko Kisiwani Pemba tunapara zetu tu Samaki na hiyo TISS tulijua ni Hoteli Kubwa.
 
Back
Top Bottom