Ni kwanini? wachina wanaweza kula nyama ya Kila na aina wapo vizuri tu?

Ni kwanini? wachina wanaweza kula nyama ya Kila na aina wapo vizuri tu?

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
4,545
Reaction score
10,426
Inashangaza sana wakuu,
Wachina, kwenye cafes, na restaurant zao wana kila aina ya nyama🥶

👉Wapo fit physically
👉Wanafanya vumbuzi nyingi
👉Wana 1.4 billion
👉Watoto wanaozaa wapo vizuri mentally

Africa nchi nyingi zina ubaguzi wa vyakula lakini, bado hatuwafikii wachina kiafya ata thinking

👉Nimepita Singida mahali nikala, mishikaki kama 12 hivi 🤣nina wasiwasi isije kua punda (wanyiramba mnisamehe)

Binafsi napenda sana Ile mentality ya wachina juu,kutokubagua vyakula just imagine
(konokono, minyoo, jongoo, tandu, Chura, paka, kenge, ) 🥶

Vipi wewe mwanajamii kwa upande wako! Una mtazamo juu kula vyakula ambavyo ata kimaandiko vilikatazwa?
 
si vibaya ukivitumia vile unavyopenda na familia yako ukizingatia baadhi yake ni free kama konokono, jongoo, chura na vingine vingi ili uwe timilifu kama wachina.
 
Kuna mahali niliuziwa mbuzi yule sio mbuzi aisee kapaja kadogo halafu nyama nyeupe nyeupe.

Nilisikilizia siku kadhaa kama nitaanza kubweka ila nilivyoona kimya nikakausha.

Sikumwambia mtu lakini.
 
Wanakula nyoka, kenge, mamba, mbwa, konokono, wale hata fisi watakula.
 
Wapemba walikua wanakula sana Ngisi haupiti mwaka tunatangaziwa wamekufa watu 12 mara watu 6 kwa Nchi ilivyo na aina nyingi za vyakula hivyi walivyokataza achana navyo tu mkuu udumavu wetu haupo kwenye chakula tu.
 
Back
Top Bottom