Ni kwanini wasiopenda Kulipa Nauli ndani ya DalaDala ( Wakwepaji Nauli ) hupenda sana Kukaa Siti za katikati tu pekee?

Ni kwanini wasiopenda Kulipa Nauli ndani ya DalaDala ( Wakwepaji Nauli ) hupenda sana Kukaa Siti za katikati tu pekee?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Je, ni kwanini Makondakta wa DalaDala nguvu zao nyingi za Kudai Nauli kwa Abiria wao huziweka sana kwa Abiria tu wa mbele na nyuma lakini mara nyingi mno wale Abiria wanaopenda Kukaa Siti za katikati hujikuta wakiwa wamesahaulika Kudaiwa Nauli? Na imegundulika pia kuwa Wakwepaji wengi wa Kulipa Nauli ndani ya DalaDala hupenda Kukaa Siti za katikati na wakizikosa hununa.
 
Cha kushangaza zaidi abiria huyo aombwapo nauli na Konda anadai "hela iko mbali ntakupatia tu" Chaajabu, abiria huyo huyo Simu ikiita anaitoa mfukoni na kuongea......

Sometimes acha Makondakta wawe wakorofi !!
 
Zipo nyingi sana ulishaziandika ,ulishaandika mpaka kuiba/kukwepa kulipa nauli kwenye daladala

Hii ina 'ufanano' upi na 'Uzi' wangu unaosema wasiopenda kulipa Nauli hupenda 'Kujificha' Siti za Kati? Halafu nikiwaita 'Wapumbavu' mnakasirika.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Umejuaje Kama napenda kupanda pikipiki [emoji12]

[emoji3059]nina kakipaji hako ka kuhisi vitu fulani kuhusu warembo,yani kwa kifupi am a ladies Man.
 
Back
Top Bottom