Ni kwanini watoto wanaogopa sindano?

jiwe gizani

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
380
Reaction score
507
Salaam wakuu,

Watoto wengi wanaogopa Sana sindano na wengi wao hawajawahi hata kuchomwa hizo sindano zenyewe lakini wanaziogopa tu.

Yaan unakuta ukiwatajia tu neno sindano wanaanza kulia na kukimbia kwa woga.

Hivi ni kwanini?
 
Mimi pia sipendi Sindano, nachoma kukiwa hamna kabisa namna nyingine.
 
Zinauma mkuu alafu inatisha adi machoni kwa kuitazama tu
 
Wazazi wengi huwajengea hofu watoto kwa kuwatishia kuwa 'ukizingua nitakupeleka uchomwe sindano'…. hii hufanya waamini sindano ni adhabu na daktari/nesi ni jitu katili.
 
sindano achana nayo kabisa, ule muda nesi anaishika shika uku anatia dawa uwii
 
Hakuna mtoto ambae hajawahi kuchomwa sindano. kachanga kabisa kanakula zake mbili za mapajani sembuse wa miaka miwili mitatu mitano etc hasa za takoni wanachomwa vizuri tu.

Sindano zinauma.
 
Siyo watoto pekee wanaoogopa sindano..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…