Ni kwanini Wazungu huvaa kishamba ilihali wana hela?

Ni kwanini Wazungu huvaa kishamba ilihali wana hela?

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3,977
Reaction score
5,339
Jamani hivi ni mimi tu niliyeliona hili au? Kwa nini Wazungu wana hela ila wanavaa kishamba? Na nguo kali zinatoka kwao.

FB_IMG_16313708616484671.jpg
 
Jamani hivi ni mimi tu niliyeliona hili au? Kwa nini Wazungu wana hela ila wanavaa kishamba? Na nguo kali zinatoka kwao?View attachment 1933620
Wao ndio wamekutengenezea nguo, wamekufundisha kuvaa eti leo unasema wanavaa kishamba. Wenzio washapita huko kwenye Kula, kulala na kuvaa saa hizi wanaangalia uwezekano wa kwenda kuishi Mars.
 
Isipokuwa kama kuna mikutano muhimu na nyeti.

Kuvaa si "issue" kwa hawa jamaa khasa huyo mwenye utajiri zaidi ya dola milioni 140 kwenye akaunti benki.

Pia umri wachangia ukiwa umepata pesa muonekano huo ni namna fulani ya kuonyesha hupendi makuu.

Ila wazungu wengine huonekana kuvaa kishamba lakini kwao nguo au mavazi ya ajabuajabu ni mitindo na ila bei kali.

Zipo nguo au mavazi yenye kuonekana yamechanika lakini hiyo ni fashion.

Tupige kazi tusake pesa.
 
Kuna level ukifikia kuna vitu vinakuwa sio issue...mafukara na wanyonge ndio wanapenda sana kujitutumua kuionyesha jamii nao wamo lakini ukweli uko palepale kuna level ukifikia huwezi kuumiza kichwa na vitu vidogo vidogo...
 
Ishu ni kwamba ukiwa masikini unataka uonekane tajiri ndio maana unajitutumua kupiga pamba kali, buti kali, saa kali, simu kali nk. "Umaridadi huficha umasikini" japo ukweli unabaki palepale kwamba wewe ni masikini.
 
Back
Top Bottom