Ni kwavile ni Chibu Diamond

Ni kwavile ni Chibu Diamond

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Imekuwa ni habari kubwa mno mpaka kwenye mashirika makubwa ya habari ulimwenguni BBC, DW nk.

Mahojiano ya Diamond kwenye kituo cha habari cha MAWINGU na 'KUKIRI' kwake kwamba mtoto w Hamisa Mobeto ni wake.

Ni kwavile ni Diamond na Zarina (hongera zake huyu binti wa KINYANKOLE anajitambua sana), LAKINI ni wangapi kati yetu tunafanya haya mambo daily? Ni wa ngapi kati yetu tunazikana mimba daily!!! Ni wangapi yetu tunazisaliti ndoa zetu na mahusiano daily???
Tuache unafique kabisa.

Tupambane na hali zetu asilimia 90% ya wanaJF hatumfikii Domo hata robo ya diamond yanawatokea wengi wetu ila hili lina mijadala mingi kwakuwa ni Diamond
 
Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.
Surely there is not a righteous man on earth, who does good and doesn`t sin.
 
Hatushangai et kisa Ni diamond.......mim nashangaa jinsi alivoshindwa kuhandle swala dgo kama Hilo na kutumia mbinu mbovu mpka jambo limelipuka vibayaaa.....swala lilikua dgo Sana Hilo kama angeamua kulihandle
 
Kivipi? Tunasubiri kuona busara zako.
 
Ndoa nyingi za hapa Bongo ziko ICU, kwa mtazamo wangu sidhani kama kuna mwanamme asiye na mke nje ya nyumba yake na pengine hata familia nyingine zaidi ya aliyenayo nyumbani kwa mkewe. Mara nyingi unakuta ni wanawak wenyewe ndio wanasalitiana, maana unakuta mwanamke anapenda jamaa atafanya kila njia ili ampate na akimpata atamfundisha jamaa namna ya kumsaliti mkewe ili asikamatwe. Mimi mwenyewe ilinitokea hii ila nilikuwa na akili, ni kweli nilimsaliti mke wangu ila baada ya kula tunda na kulia kama alivyolia Domo kitandani huku akipigwa pich na yule changudoa, nikaona ni ujinga kwani yule demu alikuwa ananifundisha namna ya kumtema mke wangu wa nda niishi na yeye. Mara niletee nguo zako kesho nizifue, sijuwi ukij kesho lazim ulale name mpaka kesho yake. Nikamshitilia mbali. Adui mkubwa wa mwanamke ni changudoa/mwanamke mwenzake.
 
Imekuwa ni habari kubwa mno mpaka kwenye mashirika makubwa ya habari ulimwenguni BBC, DW nk... Mahojiano ya Diamond kwenye kituo cha habari cha MAWINGU na 'KUKIRI' kwake kwamba mtoto w Hamisa Mobeto ni wake....
Ni kwavile ni Diamond na Zarina (hongera zake huyu binti wa KINYANKOLE anajitambua sana), LAKINI ni wangapi kati yetu tunafanya haya mambo daily? Ni wa ngapi kati yetu tunazikana mimba daily!!! Ni wangapi yetu tunazisaliti ndoa zetu na mahusiano daily???
Tuache unafique kabisa... Tupambane na hali zetu.... Asilimia 90% ya wanaJF hatumfikii Domo hata robo...! Ya diamond yanawatokea wengi wetu ila hili lina mijadala mingi kwakuwa ni Diamond
Mkuu uko sawa kabisa. Habari inakuwa habari tu pale inapomgusa mtu maarufu.
Hata hivyo Chibu anadhihirisha kuwa sisi Waafrika bado tunadumisha mila kuwa Mwanamke mmoja hatoshi. Eti tunajifichia kwenye ustaarabu wa dini ambao kimsingi umetushinda.
Wasukuma wana msemo "Bujiku bobisa Ndeji" yaani usiku au giza huficha maovu. Mambo mengi maovu wengi wetu huyafanya gizani!
Lisipojulikana wewe ni salama. Lakini kimsingi kama ingetokea kila jambo analifanya mtu chini ya jua likafunuliwa Hakika habaki mtu salama.
Mastaa huanika mambo yao. Na wasipoanikwa humulikwa muda wote , yuko wapi na anafanya nini.
Isipotokea hivyo basi mtu anaweza kutumia jina la staa kutafuta kiki.
Lakini pia sisi huku pembeni hatujui kwa nini haya yanafanyika. Yawezekana ni njia mojawapo ya hawa wenzetu ya kufanya biashara. Tunajiingiza tu bila kujua kufanikisha biashara za watu wakati ya kwetu yametushinda.
Ngoja nipambane na hali yangu.
 
Kuna mengi na magumu kwenye haya mambo, ila watu baki hupenda kushangilia magumu ya wengine bila tafakuri, huku wengine wakiongozwa na wivu tuu
 
Isingekuwa ule ushahidi wa video huyo mtoto mbona alishamkana kitambo

Asante taknolojia
 
Back
Top Bottom