Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

kulikua hamna maana ya kuujua ukoo wa yesu kama yeye alikua sio wa dunia hii.. this whole thing proves that he was a normal human being kama mimi na wewe.
 
Ndiomana nawaita mambumbumbu hoja imeletwa ni ya uhalali waJoseph kuwa na jina la Jacob au Eli mwingine huko amekuja na mambo ya uungu wa Yesu!!!

Pathetic.
 
Ndiomana nawaita mambumbumbu hoja imeletwa ni ya uhalali waJoseph kuwa na jina la Jacob au Eli mwingine huko amekuja na mambo ya uungu wa Yesu!!!

Pathetic.
hilo ilibidi akujibu huyo, mimi nimeibua swali ndani ya hilo, itakua poa ukinijibu.
 
Sichukui mambo mia at once though naweza kukujibu Yesu alikua ni mwanadamu and at the same time Mungu that's all. Anazo character za kibinadamu na kiuungu na according to His mission alitakiwa aje duniani as a human being though He's the God's second person.

Sitajadili tena hili swala mpaka nimalizane na source ya hii argument kwenye uhalali Joseph kuwa na jina la Jacob au Eli.
 
Mtu kuishi miaka 100 tu ni mziki lakini Biblia inasema Adam na Hawa waliishi miaka 900.

Je, hao walioandika Adam na Hawa waliishi miaka 900 walitumia kipimo gani?

Ipo siku utahoji baba yako alitumia kitu gani kumpa mimba mama yako hadi ukapatikana wewe Nawaza tuu kama umehoji Hivyo
 
aje duniani as a human being kuuliwa na shetani? kwanini mungu asingemuua shetani?

au ndio plan A ikifeli jaribu plan B, kwa hio plan A ya kumuua shetani ilishindikana ndo mana akaamua kumleta myahudi auwawe? is the devil that poweful?

tatizo kuu ni dhambi, unajua kama mungu mpaka sasa hivi hajatatua tatizo la dhambi pamoja na kumleta huyo myahudi?
 
Ipo siku utahoji baba yako alitumia kitu gani kumpa mimba mama yako hadi ukapatikana wewe Nawaza tuu kama umehoji Hivyo
hilo sio swala la kuhoji kwa sababu linaeleweka, watu wanahoji mambo ambayo hayaeleweki eleweki.
 
Mathayo 1:16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

Na hapo Bible ipo sawia Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa Yesu.

Bible haiseme Yusufu akamzaa Yesu popote sababu Yesu hakuzaliwa kwa mbegu za Yusufu bali kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Mariam hakukutana na mwanaume yeyote ndio Yesu akazaliwa.
 
Wewe ndio niliekuandikia hiki nataka majibu hapo chini.

Mathayo 1:13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eli-akimu; Eli-akimu akamzaa Azori;

14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eli-udi;

15 Eli-udi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaaYakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

Kwanza ujue jinsi wayahudi wanavyopeana majina ukuangalia hapo bolded nimeweka Eli hilo ni jina kamili hata kabla hujaongeza hudi au akimu hivyo enzi hizo na hata saivi mtu anaweza kuitwa let's say Michael lakini pia akitwa Mike au Elisifa lakini akaitwa Eli au Elly that's normal that's perfect.


Pili mtu anaweza kuwa na majina hata nane au saba au matano yanayoambatana la kwake la baba yake la baba mzaa baba yake la baba mzaa babu yake mpaka la ukooameyaunganisha pamoja kama majina yake.

Mfano mtu anaweza kuitwa Michael Jonathan Reuben Abraham Naton.

Huyu mtu anaweza pia kuitwa kwa kifupi Michael Naton au Michael Jonathan Naton au hata Michael Abraham it's normal it's accurate it's also very perfect.


Okay nipeni hoja yenu kuna ajabu gani Joseph au Yusufu kutumia jina la Jacob au Yakobo kama baba yake au Eli-azari au Eliazari au Hakimu kama baba yake?

Au Yesu kutumia Eli au Jacob mbona pia ametupia Mwana wa Adam au Simba wa Yuda isiwe tabu?

Am watching.
 
sasa kama ndo hivyo anakuaje na ukoo kama yeye si mbegu ya yusufu bali ni mbegu ya mungu..? hivi mimi nikikwambia nina ukoo wa kiarabu angali baba na ndugu zangu ni wangindo utanielewa?
 
sasa kama ndo hivyo anakuaje na ukoo kama yeye si mbegu ya yusufu bali ni mbegu ya mungu..? hivi mimi nikikwambia nina ukoo wa kiarabu angali baba na ndugu zangu ni wangindo utanielewa?
Yesu amewekwa kwenye huo ukoo sababu aliyemzaa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Mariam alikua ameshaposwa na Joseph na alikua automatically wa ukoo wa Joseph hata kabla ya kumzaa Yesu.

Hivyo Yesu anachukuliwa wa ukoo wa Joseph kwa bond ya Mariam mama yake na sio Joseph.

Jewish tradition ni kwamba hata kama mama yako ndio Jew na baba yako ni African automatically na wewe mtoto utakua Jew.
 
Ebu soma kwanza Luka 3:23 na Mathayo 1:16 ndipo uje hapa.
 
ukoo huwa unazungumzia BLOODLINE, na hivyo yesu sio damu ya yusufu so hawezi kubelong kwenye ukoo wake, hao waliomweka kwenye hio BLOODLINE ni wapotoshaji. ilibidi waandike "huu ndio ukoo wa yusufu, baba wa kambo wa yesu" na sio "huu ndio ukoo wa yesu kristo" huo ni upotoshaji.
 
Enzi hizo mwaka mmoja ulikuwa na siku ngapi?
hivi nami nikuulize swali hapo ni kweli hujaelewa au umeamua tu kuuliza ili uonekane na wewe umeuliza swali??
 
Ebu soma kwanza Luka 3:23 na Mathayo 1:16 ndipo uje hapa.
Luka 3:23 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli

Mathayo 1:15 Eli-udi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaaYakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

Hivyo hapo tatizo likowapi?
 
Bible haijakosewa ipo accurate 100% am going to answer each question of the thread so easy and prove the threader wrong.

I am going to start a fresh thread for the answers stay tuned.
Ukikuta mambo mawili yanapingana wazi kabisa utasemaje?

100% unajua maana yake nini?
 
Wewe unatafsiri vipi bloodline?
Hiyo niliyokuambia ndio Jewish tradition hata leo sio enzi za Yesu tu yaani unaridhi uyahudi kwa pande zote kwa baba au kwa mama nenda kajifunze ujue Jewish inheritance ndio uje uongee na mimi hapa sababu huna hata unalolijua kuhusu Jewish bloodline.
 
Nyie Wamatumbi mbona mnang'ang'ania tamaduni za watu na kusema Yesu ni Mungu wakati Wayahudi wenyewe wenye vitabu vyao mpaka leo wanamsubiri Masiha?

Hivi inaingia akilini Wazungu waseme Mwanamalundi ni Mungu halafu Wasukuma wenyewe waliomuina tangu anazaliwa mpaka anakufa waseme si Mungu?
 
Luka alisema Yusufu alikuwa mwana wa ELI(hakumtaja Yakobo)...Mathayo akasema Yosefu alikuwa mwana wa Yakobo,(hakumtaja Eli)...sasa wewe unasema Yusufu alikuwa mtoto wa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…