Mkuu, suala lako limepata mtaalamu wa uzazi.
Utangulizi:
Mosi tambua kwamba,siku ambayo ulifanya mapenzi na kimada wako ni siku ya 15 katika mzunguko wake wa hedhi.
Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida yaani siku 28, kwake hiyo ni siku ya hatari.
Labda nikupe kanuni rahisi ambayo itakusaidia wewe na wengineo.
N - 14days = M
N = Jumla ya siku ambazo mwanamke anatumia kutoka bleed moja hadi nyingine au Jumla ya siku za mzunguko mmoja wa hedhi.
M = Siku ambayo yai hupevuka na kuwa tayari kurutubishwa.
Sasa kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida ambao ni siku 28, kanuni itatumika kama ifuatavyo:
N = 28 , je M = ?
N - 14 = M
28 - 14 = 14
Hivyo mwanamke huyu siku yake ya upevushaji yai ni ile ya 14.
Hivyo tumia kanuni hiyo kwa mwanamke yoyote mwenye idadi ya siku za mzunguko zozote.
Siku za hatari ni zipi?
Siku za hatari ni hizi M - 3, M - 2, M - 1, M, M + 1, M + 2, M + 3.
Ila binafsi huwa nashauri kuwa salama zaidi, mtu asifanye mapenzi siku 5 kabla na baada ya siku ya upevushaji wa yai.
Ushauri;
Muulize kimada wako idadi ya siku zake za mzunguko halafu tumia kanuni hiyo.