Ni kweli anavyodai SATIVA kuwa Mtandao wa Simu (Halotel) umehusika 'kumuuza' Humphrey Polepole?

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
​
Stori ya Humphrey Polepole kutekwa naona inazidi kushika kazi ndugu zangu, kuna sehemu nimekuta hii screenshot, je inawezekana ni kati ya vitu vilivyomfanya akanaswa? Namba ya simu inayotajwa kutumika ni ya Mtandao wa Halotel na imesajiliwa kwa jina la Humphrey Herson Polepole.

Kampuni ya Halotel inatajwa na SATIVA kupitia Mtandao wa X (Twitter) kuwa imehusika katika kucheza mchezo kabla ya watekaji kumnasa Polepole.

Je ni kweli imehusika, nadhani hii ni nafasi ya Mtandao wa Halotel kujitokeza na kusema neno, kuna mamilioni ya Watanzania wanaotumia Mtandao huo kama si kweli au ni kweli ili Watumiaji wajue "status" ya Mtandao wao na matumizi yao yaweje.

​
SATIVA kaandika kuwa “Mtandao wa simu "HALOTEL" ndio waliomuuza POLEPOLE.

"Hiyo picha ni code ya muamala ambayo Pole Pole alimtumia hela ya kodi mama mwenye nyumba kwa mtandao wa HALOTEL.

"Wakamtafuta mama mwenye nyumba awaonyeshe jamaa alipo, akaenda kama kukagua nyumba na kuwaambia wasaidizi wale wawili wa PolePole kuwa usiku waondoke maana kuna watu watakuja wanamtaka PolePole hivyo wasiwepo ili kuondoa ushahidi, kama wakibaki watachukuliwa na wao."
 
Wabongo bhana, Sasa hapo mbona n kama n mtu mwingine ndo anamtumia pesa polepole, n sawa na mm nichukue hy namba yake afu nitume pesa, Sasa hapo Kuna taarifa gani za polepole mpaka kushikwa?
Kwan Kuna mtandao wa simu hawajui watumiaji wake mpaka wakae kusubiri miamala kufanyika?

Sasa hv kila mtu ni CIA
 
Au wewe ndio ulikuwa unataka kumtumua hiyo 20000 kabla ya kutuma uka screenshot, sio kitu cha msingi hapo.
 
Sidhani kama ni kweli yaani yeye mwenyewe ajihatarishe kutuma muamala live , nadhani hata Mama mwenyewe nyumba wake huenda alikuwa hajui kuwa anaishi mule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…