Kijukuu cha Tanzania
Member
- Dec 6, 2025
- 7
- 5
Tangu tarehe 1 Aprili 2026, baada ya EWURA kutangaza kupanda kwa bei ya mafuta nchini, hali imekuwa ngumu kwa wananchi wengi, hasa wafanyakazi wanaotegemea usafiri wa umma kila siku.
Ni ukweli usiopingika kuwa bei ya mafuta imeongezeka. Hata hivyo, baadhi ya watoa huduma wa vyombo vya usafiri wanaonekana kutumia fursa hiyo kuongeza nauli kwa kiwango kisichoendana na uhalisia wa ongezeko lenyewe.
Hapa Mbeya hali ni mbaya sana nauli zimepanda kiholela na kuwa juu mno, Kwa mfano, nauli iliyokuwa shilingi 4,000 sasa imepanda hadi shilingi 8,000 ongezeko la zaidi ya mara mbili. Hali ni hiyo hiyo hata kwa usafiri wa bajaji; hapa Mbeya, nauli iliyokuwa shilingi 800 imefikia hadi 2,000.
Nauli za Mbeya-Kyela, Mbeya-Tukuyu hazishikiki. Watoa huduma wa usafiri wameamua kutumia hii fursa yabkupanda bei ya mafuta ili kujinufaisha wao, jambo ambalo linatuumiza sana watumiaji wa usafiri wa umma.
Tunatambua kuwa gharama za uendeshaji zimeongezeka kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo imeongezeka kwa wastani wa shilingi 900 hadi 1,000 kwa lita. Lakini je, ni haki kwa nauli kupanda kwa kiwango kikubwa kiasi hicho?
Ni muhimu tukumbuke kuwa mishahara ya wafanyakazi haijaongezeka. Hivyo basi, mzigo huu mkubwa unaangukia moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida.
Tunatoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuzingatia haki na utu. Tuhurumiane katika kipindi hiki kigumu. Faida ni muhimu, lakini ustawi wa jamii ni wa msingi zaidi.