Ni kweli Derby imepoa?

Ni kweli Derby imepoa?

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Kuna mjadala unaendelea mitandaoni juu ya hali ya hamasa kuelekea mechi ya kesho.

Mashabiki wengi wa Simba pamoja na viongozi wao wanasema derby hii imepoa kwa sababu wao sio wenyeji na hawajahusika kwenye promotion ypa mchezo.

Mashabiki wa Yanga wanasema derby haijapoa. Lakini kwa nionavyo mimi derby hii imepoa na sababu kuu ni upande wa Simba kutojiamini kama watatoka salama.

Hakuna kingine
 
sisiiiiiii tuna uchungu na Timu Siiiii tuna uchungu na timu wew na GSM nani ana uchungu na Timu umepewa elfu kumi ya Nauli na Mjombaa unakuja uwanjaa unavunja Geti unabakisha elfu tano unaweka Bando unakuja mtandaoni unaza kutukanaa watu sisiiiiii tunachungu Sisiiiiiii tuna uchunga sisi vijana bwana tutaftie hela wengineee mlala njaa sisiiiiii tuna uchungu na timu sisiiiiii tuna uchungu na Timu
 
Derby inachezwa na wazee wanakesha kiringeni hakuna kulala wanapishana anga za b.mkapa na wengine wameingia kabisa uwanjani bila kuonekana
 
Ukweli derby imepoa sanaaaaaa na ni ukweli mchungu sababu Simba ni kama hana habari nayo,
Msimu huu Yanga ni kama amemaliza show vzr tu, na bado ametupiga kono la nyani, sa tuhangaike na nini?

Kombe la Yanga, mechi ya Yanga, mpinzani favorite kushinda ni Yanga, lakini bado imepoaaaa kama maji mtungini.

Jamani tuacheni Simba tuko bize kwanza na viongozi wetu na maandalizi ya AFL
 
Kuna mjadala unaendelea mitandaoni juu ya hali ya hamasa kuelekea mechi ya kesho.

Mashabiki wengi wa Simba pamoja na viongozi wao wanasema derby hii imepoa kwa sababu wao sio wenyeji na hawajahusika kwenye promotion ypa mchezo.

Mashabiki wa Yanga wanasema derby haijapoa. Lakini kwa nionavyo mimi derby hii imepoa na sababu kuu ni upande wa Simba kutojiamini kama watatoka salama.

Hakuna kingine
Sasa team mashabiki wao wanaingia bure kiufupi yanga haijawahi kujaza taifa.
 
Back
Top Bottom