Jayfour_King
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 1,135
- 130
Wana Baraza,
ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la wazazi wa kitanzania kupeleka watoto wao kwenda kupata elimu ya viwanngo mbalimbali nchini Uganda na Kenya.
Mada hii lengo lake ni kujadili ubora wa elimu ipatikanayo nchini Uganda kwa wanafunzi wa kitanzania.
Najaribu pia kuangalia anguko la mifumo mingi katika jamii yoyote hutokana na anguko la kiuchumi , hivyo basi nahusiha kuanguka kwa uchumi wetu kwa asilimia nyingi kulitokana na vita ambavyo sisi kama watanzania tulipigana na Uganda 1978/79 na watanzania kuibuka washindi na kufanikiwa kumtimua Idd Amin Dada madarakani.
Tathimini yangu inanifikirisha kwamba tulioshinda vita ndio ambao ingetegemewa kwamba mifumo yake mingi kutoathiriwa kwa kiasi kikubwa na zoezi zima.
Bahati mbaya kwamba hali halisi ni kinyume.
Mimi nitapenda zaidi kujadili suala la elimu.
Katika hali ya kawaida ingetegemewa kwamba, sisi tulioshinda vita ile mingi ya mifumo yetu ingekuwa haijaathirika kama ya walioshindwa na hivyo mifumo yetu ingebaki kuwa ile ile tuliyokuwa tumepanga hapo awali.
Kutokana na anguko la elimu tulilonalo sasa najaribu kufikiri kwamba, pengine tatizo ni kwamba mfumo wetu wa elimu ulikuwa mbaya tangu awali bila kujali Kigezo chochote nilichoeleza hapo juu (vita) na hivyo kwa vyovyote vile tungefikia anguko tulilofikia sasa na kwamba lilikuwa ni suala la wakati tu, bila kujali nini kilitokea.
Katika hali ya kawaida utulivu na amani tuliyokuwa na tuliyo (kama tunavyo) tangu tupate uhuru wetu na hata jinsi uhuru wenyewe ulivyopatikana katika mazingira ya amani ingetegemewa kwamba tungekuwa bora zaidi kulinganishwa na nchi yoyote ya iliyokuwa Jumuiya ya Africa Mashariki wakati huo (nchi tatu).
Wana JF naomba maoni yenu kuhusu hili (Elimu) yetu TZ kwa kulinganisha na Uganda na Kenya na si vibaya kama uchambuzi utatuelekeza kwenye uchumi pia ili iwe rahisi kujiuliza tulikwama na bado tumekwama wapi?
NAWASILISHA.