Ni kweli elimu ya Uganda iko juu?

Ni kweli elimu ya Uganda iko juu?

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Posts
1,135
Reaction score
130
Wana Baraza,
ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la wazazi wa kitanzania kupeleka watoto wao kwenda kupata elimu ya viwanngo mbalimbali nchini Uganda na Kenya.

Mada hii lengo lake ni kujadili ubora wa elimu ipatikanayo nchini Uganda kwa wanafunzi wa kitanzania.

Najaribu pia kuangalia anguko la mifumo mingi katika jamii yoyote hutokana na anguko la kiuchumi , hivyo basi nahusiha kuanguka kwa uchumi wetu kwa asilimia nyingi kulitokana na vita ambavyo sisi kama watanzania tulipigana na Uganda 1978/79 na watanzania kuibuka washindi na kufanikiwa kumtimua Idd Amin Dada madarakani.

Tathimini yangu inanifikirisha kwamba tulioshinda vita ndio ambao ingetegemewa kwamba mifumo yake mingi kutoathiriwa kwa kiasi kikubwa na zoezi zima.

Bahati mbaya kwamba hali halisi ni kinyume.
Mimi nitapenda zaidi kujadili suala la elimu.

Katika hali ya kawaida ingetegemewa kwamba, sisi tulioshinda vita ile mingi ya mifumo yetu ingekuwa haijaathirika kama ya walioshindwa na hivyo mifumo yetu ingebaki kuwa ile ile tuliyokuwa tumepanga hapo awali.

Kutokana na anguko la elimu tulilonalo sasa najaribu kufikiri kwamba, pengine tatizo ni kwamba mfumo wetu wa elimu ulikuwa mbaya tangu awali bila kujali Kigezo chochote nilichoeleza hapo juu (vita) na hivyo kwa vyovyote vile tungefikia anguko tulilofikia sasa na kwamba lilikuwa ni suala la wakati tu, bila kujali nini kilitokea.

Katika hali ya kawaida utulivu na amani tuliyokuwa na tuliyo (kama tunavyo) tangu tupate uhuru wetu na hata jinsi uhuru wenyewe ulivyopatikana katika mazingira ya amani ingetegemewa kwamba tungekuwa bora zaidi kulinganishwa na nchi yoyote ya iliyokuwa Jumuiya ya Africa Mashariki wakati huo (nchi tatu).


Wana JF naomba maoni yenu kuhusu hili (Elimu) yetu TZ kwa kulinganisha na Uganda na Kenya na si vibaya kama uchambuzi utatuelekeza kwenye uchumi pia ili iwe rahisi kujiuliza tulikwama na bado tumekwama wapi?

NAWASILISHA.
 
Itabidi baadaye turudi na kuangalia elimu maana yake ni nini hasa.
Ama sivyo, Ukilinganisha Tanzania,Kenya na Uganda ni kwamba mfumo
wa elimu wa Tanzania unaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, Kenya na Uganda
wanaendesha mfumo wao kwa Lugha ya Kiingereza.

Tanzania haijafanikiwa kujenga uchumi unaojitegemea, uchumi wetu umekuwa
ni tegemezi kwa nchi za magharibi na Marekani, hata huo mfumo wetu wa elimu
ya kiswahili unafadhiliwa na kuendeshwa na mfumo wa nchi za ulaya na marekani
ambao hutumia kiingereza, kama ilivyo kwa kenya na uganda.

Hivyo ukiwapima watanzania, wakenya na waganda au wale waliopita kwenye
mifumo ya elimu ya mataifa haya, watanzania wanaonekana wako nyumba
sababu wamo katika mfumo wa kiingereza ambako hawakujiandaa na wala
hawajiandai kuuishi. Hivyo tatizo kubwa ni mawasiliano tu.

Ndio maana mwanzoni nimesema kwamba baadaye turudi na kuangalia elimu
maana yake ni nini hasa, sababu hata hao wazazi wa kitanzania wanaopeleka
watoto wao kenya na uganda ukiwauliza kwa nini wanafanya hivyo watakuambia
ni kwa sababu huko watoto wanapata elimu bora inayopimwa kwa uwezo wa watoto
hao ama kuongea au kuongea na kuandika kiingereza, na kweli wamefanikiwa.
 
Inawezekana ni taarifa za zamani kidogo. Kwa hakika mitaala mingi ya elimu kwa Africa yote inatakiwa ibadilike ili iende sambamba na matakwa ya waajiri.

Muelekeo wa dunia na mabadiliko ya hali halisi ktk kila nyanja siasa, uchumi na jamii inalazimisha kubadilisha maana nzima ya elimu. Kwa mfano theories zinazotumika hata ktk baadhi ya maabara zetu ni za kizamani sana. Haiwezekani ktk wakati tulionao kumfundisha mtu kwa theory kutumia Viza card na mengineyo.

Inawezekana Uganda au Kenya zikawa bora kama tukisema elimu ni kuzungumza kingereza kizuri lakin kwa maendeleo Tanzani inapiga hatua kama itamaliza baadhi ya matatizo kama umeme, transparency, accountability na good governance.
 
Hilo halina ubishi mkuu,

Katika nchi za africa mashariki quality ya elimu iko hivi.

1. Kenya
2. Uganda
3. Rwanda
4. Tanzania
5. Burundi

Hivi unajua wasomi "voda fasta" tunaovuna pale chuo kikuu cha kata mlimani dar hawajui hata kujielezea, siyo kwa kimombo tu hata kwa kiswahili, upeo mdogo unajiuliza hivi kweli huyu ni uni graduate kweli?..
 
Jiulize kwanini hapa Tanzania huwa tunaita wataalamu wengi wa kompyuta kutoka Uganda au Kenya kuja hapa nchini kerekebisha mitambo yetu...mfano Tanga Cement mwezi wa 8 walileta mtaalamu kutoka kampala kuja kurekebisha mfumo wa fibre optics...hahaaaa
 
Jiulize kwanini hapa Tanzania huwa tunaita wataalamu wengi wa kompyuta kutoka Uganda au Kenya kuja hapa nchini kerekebisha mitambo yetu...mfano Tanga Cement mwezi wa 8 walileta mtaalamu kutoka kampala kuja kurekebisha mfumo wa fibre optics...hahaaaa

Sijui kinachokuchekesha hapo ni nini?

Sina haja yakujiuliza kwa nini wameleta mtaalamu kutoka Uganda, hiyo ni internal policy yao na huyo Mganda sio lazima akawa amesoma huko Uganda.

Na utathibitishaje kuwa alipata contract hiyo ya fibre optics kwa Uganda wake au ...?

GT go more than that....
 
Back
Top Bottom