GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nimeshasikia hivyo tokea nikiwa mdogo, lakini kama si sahihi kwa asilimia mia moja.
Kwenye nchi hii, kuna watu ambao ni kama vile hawagusiki, haijalishi watakachofanya! Hapo siwaongelei viongozi, bali vigogo wanaoweza kuonekana kama vile wameiweka Serikali mfukoni.
Kikatiba, Rais wa Tz hashtakiwi akiwa madarakani na hata baada ya kutoka madarakani!
Kama ndivyo, hata akiamua kufanya kosa la jinai hatachukuliwa hatua zozote za Kisheria?
Chukulia kwa mfano, Rais aliyeko madarakani akiamua kumpiga mtu risasi hadharani kuna mtu atakayethubutu kumchukulia hatua?
Hivi kwa mfano, Rais mstaafu, Kikwete, akigombana na mtu, labda jirani yake, na (Kikwete ) akaamua kumtukana, anaweza kuchukuliwa hatua zozote?
Nimeuliza kwa sababu ninataka kufahamu! Naomba nisituhumiwe kuwa ninauliza maswali mepesi. Majibu yake yana umuhimu mkubwa sana kwangu.