Ndugu zangu, kuna ukweli hapa kuwa ukiwa na roho nzuri sana, ni nadra sana kufanikiwa kimaisha?
Binafsi kwangu naona ili ufanikiwe kimaisha pale unapopata nafasi, kazi/ biashara inayokupa kipato unapaswa kuwa katili sana.
Ukatili huu ni kuwa na roho mbaya kwenye pesa, yaani siyo kila mtu akija kukuomba wewe unamwaga tu chukua.
Siku ukikosa kazi au biashara kuyumba hakuna rangi utaacha ona kwenye hii dunia.
"Been granting wishes like a genie..."
Pusha T - "If You Know, You Know".
Natoka kumrushia mtu $100 hapa sasa hivi, nakutana na hii mada.
Jana Vodacom wamezingua sana kwenye M-Pesa through Sendwave. Imebidi nisubiri usiku mzima ndiyo asubuhi hapa naona message wamerudi online baada ya kuwa hawapatikani.
Hiyo $100 kwangu hata kutoka dinner na mtu haitoshi, my dinners for two or three people are typically around $200, depending on the restaurant. Lakini kwake inamsogeza sana tu, inaweza kuwa suala la life or death.
Na kuwa mtoaji hakujawahi kunifanya niwe masikini. In fact naweza kusema majukumu zaidi yananiongezea ubunifu wa kuwa vizuri zaidi kiuchumi.
Leo hii na close deal kubwa tu New York City.
Ni kanuni ya maisha kuwa hutakiwi kula peke yako unachochuma peke yako. Vinginevyo vizazi vitakwisha.Hata wewe kuna wakati ulisaidiwa.
Ninachofanya mara zote ni kuongeza bidii ya kazi, biashara na ubunifu kiasi kwamba isiwe shida kwangu kuwa mtoaji. Niwe nazalisha kwa kasi na amount kubwa mpaka hela ninayotoa isiweze kuniathiri.
Kingine, hutakiwi kutoa kwa kila mtu, kuna watu fulani ambao wanastahili kupewa. Na hata hao walio katika circle ya kustahili kupewa, wanatakiwa kuwa na justification.
Ukitoa kwa kila mtu, bila mahesabu, na wewe utaishia kuwa ombaomba tu uwe mzigo kwa wengine.
Waswahili walisema, mali bila daftari, hupotea bila habari.
Kikubwa ni kuwa na balance, kuwa na bajeti unayojiwekea kuwa nitasaidia watu wanaostahili kwa kiasi fulani. Wengine wataita sadaka, wengine wataita paying it forward, ni kusaidiana tu.
Pia, unatakiwa kujua kukataa kusaidia bila kujisikia vibaya ikiwa hali hairuhusu au unaelekea kuvuka bajeti yako uliyojipangia kusaidia watu.
Mimi si tajiri, lakini najua matajiri wote wa kweli wanajua kusaidia.