Ni kweli ili ufanikiwe kimaisha unapaswa kuwa na roho mbaya?

Kimsingi hakuna mtu ambaye si mtoaji, hata yule unayemuona ni mbinafsi sana kuna watu wake wa karibu anawasaidia kwa namna flani.

Binafsi naona kuwa mchoyo 100% haiwezekani, kila mtu ana soft-spot.

Na kuhusu kumsaidia kila mtu, hilo haliwezekani pia utakuwa unafuja mali. Hata hivyo haiwezekani kila unayemfahamu akawa na shida kila siku, na anazileta kwako.
 
Reactions: Tui
Nafikiri issue apa unazungumzia nidhamu ya pesa kwa sababu roho mbaya inaweza pia kufanya utumie pesa ovyo kuonyesha hiyo roho mbaya yako.
Ukikunja sura na kuwa na sura ngumu wakati wote hakuna KENGE yoyote atakayethubutu kukusogelea kukupiga mzinga.
 
Ukikunja sura na kuwa na sura ngumu wakati wote hakuna KENGE yoyote atakayethubutu kukusogelea kukupiga mzinga.
Hata wakikupigia simu au SMS wataona hiyo ndita uliyokunja?Just joking.
 
Ni kwl sio kila anayekuja kwako anataka pesa basi ni wa kumpa,,

Wengine chuma ulete.
 
Ni kweli,Kwa ambao hatuna roho mbaya tunawezaje kuwa na roho mbaya ili tupate mafanikio
 
Siamini katika roho mbaya, naamini ktk kupemba hela kuliko kitu chochote kile
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli.

Vijana wengi baada ya kupata kazi, FAMILIA aliyotokea ndio humtolea Macho, ataombwa hela za kila aina.

Kwa mawazo ya kimaskini tutasema usiposaidia ndugu hasa wa familia moja ni mbaya. Ila kiuhalisia si sawa baada ya kujipata tu uanze kutoa misaada mikubwa mikubwa hali ya kuwa wewe binafsi hujajiimarisha kiuchumi.

Ni ukweli mchungu ambao watu wengi hawakubaliani nao. Pata kazi jijenge uwe vzr kiuchumi ndio unyanyue hao wengine. Ukijifanya mtakatifu saana lazima uendelee kuwa maskini tu.

Mshahara wenyewe laki 5 unatak usomeshe.. umjengee Baba nyumba, Mama umpe hela ya vitenge.. etc
 

Majibu yote ya huu uzi yako hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…