Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Naungana kabisa na mheshimiwa Rais, kwenye suala la katiba hatupaswi kuwa na haraka kwa kujilinganisha na nchi nyingine.
Vivyo hivyo hata kwenye masuala ya ukusanyaji wa kodi hatupaswi kujilinganisha na 'wenzetu Indonesia, Japan, Austraria' nk maana ni kweli hatufanani!
Mara kadhaa tumekuwa tukiwasikia viongozi wa serikali wanapotaka kusisitiza jambo fulani husema, "kwa mfano wenzetu Marekani...!"
Hivyo basi ili kusudi suala hili likae sawa, si tu kwenye mabadiliko ya katiba kujilinganisha na wenzetu Kenya, bali hata kwenye masuala mengine ikiwa ni pamoja na njia za ukusanyaji wa kodi na makato mengine. Nchi yetu bado inahitaji elimu kabla ya utekelezaji!
Naomba kuwasilisha!
Ndimi mbunge ajaye!