Ni kweli kiwango cha kukosa ajira nchini ni 7.8% kama takwimu za NBS zinavyosema?

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo nimetembelea tovuti ya NBS, katika pititia pitia nimeona kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kipo asilimia 7.8, takwimu ambazo zilikusanywa kutoka kwenye sensa ya watu na makazi. Chapisho husika limetolewa Feb, 2024.

Nauliza hizi asilimia za NBS zinaakisi uhalisia uliopo kwa ground? Kwamba katika kila watanzania 100 wenye uwezo wa kufanya kazi, ni 7 pekee hawana hizo kazi! Zile ratio kubwa za wanaoenda kwenye interview kulinganisha nafasi zinazotangazwa, wale watu huwa wanatoka wapi?

Unemployment Tanzania - Copy.png
 
Hawatoweza kutatua tatizo la ajira na mengine luluki kwa sababu kuu wahusika wanapenda kujiongopea.

Yaani Tanzania ni kama France yenye unemployment rate 7.5% au uchumi wetu ni inclusive karibu na Eurozone yenye average ya unemployment rate 6.3%.

Wao wakipewa leeway basi wanaitumia vibaya kutengeneza takwimu.

Ukisoma mada za watu wanaosherekea diaspora kurudishwa na ajira zitakazopotea kwa kukatwa misaada ya US; hali ni mbaya.

Kwa sasa ajira Tanzania ni bahati (kudra za mungu) kwa mtazamo wa vijana; jambo ambalo linaleta wivu kwenye jamii. Ni hatari ukisoma michango ya mada kadhaa.

Yaani wewe ukisikia fulani ni HR basi kwenye kichwa chako ndio mtu anaetoa kibali cha kutoa ajira kwenye taasisi na hiyo kampuni inaajiri all year round.
 
Data nyingine nizakupika tu! kwa lipi? Kuna wengi sana wapo mitaani wana vioski na machinga mitaani lbda ndo ajira wenyewe. Hatuambie ukweli kama vipi tusiwe tunahangaisha vichwa na maelimu uchwara na ajira uchwata.
 
Leo nimetembelea tovuti ya NBS, katika pititia pitia nimeona kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kipo asilimia 7.8, takwimu ambazo zilikusanywa kutoka kwenye sensa ya watu na makazi. Chapisho husika limetolewa Feb, 2024.

Nauliza hizi asilimia za NBS zinaakisi uhalisia uliopo kwa ground? Kwamba katika kila watanzania 100 wenye uwezo wa kufanya kazi, ni 7 pekee hawana hizo kazi! Zile ratio kubwa za wanaoenda kwenye interview kulinganisha nafasi zinazotangazwa, wale watu huwa wanatoka wapi?

Ndiyo. Mama is doing bettre. During the ********'s regime unemployment was 100%
 
Leo nimetembelea tovuti ya NBS, katika pititia pitia nimeona kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kipo asilimia 7.8, takwimu ambazo zilikusanywa kutoka kwenye sensa ya watu na makazi. Chapisho husika limetolewa Feb, 2024.

Nauliza hizi asilimia za NBS zinaakisi uhalisia uliopo kwa ground? Kwamba katika kila watanzania 100 wenye uwezo wa kufanya kazi, ni 7 pekee hawana hizo kazi! Zile ratio kubwa za wanaoenda kwenye interview kulinganisha nafasi zinazotangazwa, wale watu huwa wanatoka wapi?

Kwanza kabisa, hata kama data hizo zingrkuwa kweli zimetoka kwenye sensa, data za kutoka kwenye sensa zishapitwa na wakati. Ni zaidi ya miaka miwili kutoka sensa ya 2022.

Data za unemployment zinatakiwa kupatikana kila mwezi. Hizo data za sensa zishapitwa na wakati. Tanzania ina watu wengi sana, kila mwaka population inaongezeka kwa takriban 4%

Pili, data za kwenye sensa wamezihakiki vipi?
 
Leo nimetembelea tovuti ya NBS, katika pititia pitia nimeona kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kipo asilimia 7.8, takwimu ambazo zilikusanywa kutoka kwenye sensa ya watu na makazi. Chapisho husika limetolewa Feb, 2024.

Nauliza hizi asilimia za NBS zinaakisi uhalisia uliopo kwa ground? Kwamba katika kila watanzania 100 wenye uwezo wa kufanya kazi, ni 7 pekee hawana hizo kazi! Zile ratio kubwa za wanaoenda kwenye interview kulinganisha nafasi zinazotangazwa, wale watu huwa wanatoka wapi?

Kuna misconception kubwa watu kujaa kwenye interview, nakumbuka interview moja nilienda watu kma 1000 hivi ila wengi mnoo walikua na vìbarua ila walitaka tu job security ya serikalini.

Hata mimi muda wa sensa nilikua sina ajira ya kudumu nilikua nafundisha kama part timer so nilirekodiwa kama "nina ajira".

Changamoto nyingine ya takwimu ni kwamba hata ukisema umejiajiri inahesabika ni ajira, ukisema ni boda au muuza karanga nayo ni ajira!!

Kingine wale wenye elimu ndogo, wazee na walio under 18 wakikosa kazi hawahesabiki hawana kazi maana "hawaajiriki". So mambo ya takwimu lazima ujue criteria gani ilitumika ku define "employment".
 
Wenzake wametumia kodi za wananchi kufanya tafiti wakapata ratio ya 7%,nayeye aingie field afanye tafiti kwa hela yake.
Sasa huu ukubwa wa tatizo la ajira unaoongelewa bungeni, watendaji wa Serikali etc unatoka wapi kama kiwango cha tatizo la ajira kipo chini hivyo?
 
Leo nimetembelea tovuti ya NBS, katika pititia pitia nimeona kiwango cha ukosefu wa ajira nchini kipo asilimia 7.8, takwimu ambazo zilikusanywa kutoka kwenye sensa ya watu na makazi. Chapisho husika limetolewa Feb, 2024.

Nauliza hizi asilimia za NBS zinaakisi uhalisia uliopo kwa ground? Kwamba katika kila watanzania 100 wenye uwezo wa kufanya kazi, ni 7 pekee hawana hizo kazi! Zile ratio kubwa za wanaoenda kwenye interview kulinganisha nafasi zinazotangazwa, wale watu huwa wanatoka wapi?

Mmh hiyo 7.8 labda wameangalia walimu watoro tu makazini ila kwa issue ya kazi Tanzania hizo takwimu wanazitolea wapi ikiwa serikali haina data za nguvu kazi zake imagine kurudisha mkopo tu kwa waliokopa HESLB hadi wawatangazie kwenye magazeti kwamba mjitokeze it's meant that hata data za waliowakopesha hawana sasa utakuwaje na data za watu ambao hujui hata kama waliomba ajira au lah..
Bongo michosho sana.
 
Kuna misconception kubwa watu kujaa kwenye interview, nakumbuka interview moja nilienda watu kma 1000 hivi ila wengi mnoo walikua na vìbarua ila walitaka tu job security ya serikalini.

Hata mimi muda wa sensa nilikua sina ajira ya kudumu nilikua nafundisha kama part timer so nilirekodiwa kama "nina ajira".

Changamoto nyingine ya takwimu ni kwamba hata ukisema umejiajiri inahesabika ni ajira, ukisema ni boda au muuza karanga nayo ni ajira!!

Kingine wale wenye elimu ndogo, wazee na walio under 18 wakikosa kazi hawahesabiki hawana kazi maana "hawaajiriki". So mambo ya takwimu lazima ujue criteria gani ilitumika ku define "employment".
Kipimo cha unemployment ni idadi ya watu ambao are actively looking for employment.

Sio wabangaizaji ambao wanafanya lolote mradi mkono uende kinywani.

Kuzunguka na fyekeo mtaani na kuomba mungu atokee msamaria mmoja akupe gig ya kukata majani yake siku nzima kwa tsh 5000 sio ajira rasmi.

Kwenda sokoni na kuombea lorry la mizigo lije upate tender ya kuwa kuli sio ajira.

Idadi ya watu wanaoenda kwenye kuomba kazi inapotangazwa hiko ndio kipimo cha mahitaji ya kazi, sasa aina maana wengine sio wabangaizaji sehemu zingine ya kwamba wapo idle tu.

Tatizo la ajira Tanzania ni time bomb, akitokea political demagogue ambae kweli anaweza cheza na psychology za vijana.
 
Mtoa mada atofautishe ajira na kazi, watu wengi sana wana kazi zao za kuingiza kipato, hawajaajiriwa
Bodaboda ni kazi ya kuingiza kipato ila sio ajira?
 
Kipimo cha unemployment ni idadi ya watu ambao are actively looking for employment.

Sio wabangaizaji ambao wanafanya lolote mradi mkono uende kinywani.

Kuzunguka na fyekeo mtaani na kuomba mungu atokee msamaria mmoja akupe gig ya kukata majani yake siku nzima kwa tsh 5000 sio ajira rasmi.

Kwenda sokoni na kuombea lorry la mizigo lije upate tender ya kuwa kuli sio ajira.

Idadi ya watu wanaoenda kwenye kuomba kazi inapotangazwa hiko ndio kipimo cha mahitaji ya kazi, sasa aina maana wengine sio wabangaizaji sehemu zingine ya kwamba wapo idle tu.

Tatizo la ajira Tanzania ni time bomb, akitokea political demagogue ambae kweli anaweza cheza na psychology za vijana.
Vipi kuhusu madalali na mawinga?
 
Back
Top Bottom