Ni kweli kuna malaika anaitwa Israili ambaye ndiyo mtoa roho?

Ni kweli kuna malaika anaitwa Israili ambaye ndiyo mtoa roho?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Tangu nakua mpaka leo nimezeeka, nimekuwa nikisikia watu wakisema kuwa "malaika mtoa roho anaitwa Israili".

Sina hakika kama huyo Israili jina lake linatokana na jina Israel au lah.

Kwa watu wajuzi wa mambo ya kiroho naomba mnisadie kujua kama kweli malaika mtoa roho anaitwa Israili.
 
Malaika aliyewakilishwa kwa kazi hiyo anaitwa malaika wa mauti, ni malaika mwenye nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya kazi ya kutoa roho nyingi kwa wakati mmoja nae ana wasaidizi wake, wao hutoa roho kuanzia kwenye vidole vya miguu kisha mpaka karibu au usawa wa mitulinga kisha yeye anamalizia.

Ni malaika mtukufu na siku ya mwisho na yeye atakufa pia, haitwi israeli, na si kweli kuwa anaitwa hivyo, anawajua watu wote na anajua nani siku yake imefika kwani anapewa utaratibu muda ukifika ila kabla hajui, hawahi wala hachelewi.

"Waambie: Atakufisheni malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha kwa mola wenu mtarejeshwa."
Qur'an 32:11
 
K

Kama haitwi Israel anaitwa nani?
 
Malaika Mtoa Roho anaitwa Azrael
Screenshot_20240620-095017.jpg
 
K

Kama haitwi Israel anaitwa nani?
Kwani hapo mwanzo hapasomeki mkuu? nimesema anaitwa malaika wa mauti hilo ndo jina lake, israeli ni jina la nabii yaaquub baba wa wana wa israeli na israeli ndo yeye mwenyewe, na maana ya israeli ni mja wa allah yaani abdullah kwa lugha ya kihebrania, sasa iweje malaika wa mauti avalishwe hilo jina lisilomuhusu.
 
Baada ya wadau kutoa maoni yao, kama bado hautoelewa basi usiwe na wasiwasi mkuu, subiri siku atakapo kuja kwako ndipo umuulize jina lake sahihi.
 
Back
Top Bottom