Wadau,
Tumeenda kituo cha afya Kanyala kilichopo halmashauri ya Geita Mji kwa nia ya kumpatia chanjo ya awali mtoto mchanga. Wahudumu wa afya wametuambia mtoto ataruhusiwa kupata matone tu ya kuzuia polio lakin chanjo nyingine hawezi kupata.
Wahudumu hao ambao walinisubirisha kwa zaidi ya masaa mawili wakinywa chai, waliniibia siri kuwa eti mambomba waliyoyataja kwa jina la BCG yameadimika mno, hayapatikani sehemu kubwa ya kanda ya ziwa.
Wameitaja na Hospitali moja kubwa sana iliyopo jijini Mwanza eti nayo haina mabomba hayo japo dawa ipo. Mtoto kaambulia kupata matone tu na chanjo kaambiwa awe anafuatilia kama mabomba hayo yameshakuja.
Sijaambiwa hata kuacha namba ya simu ili yakija wanipigie. Kuna mwenye ukweli wa hizi taarifa? Nimejisikia vibaya sana kwa tulipofikia.