- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na machapisho kadha wa kadha kumuhusu kunguni katika moja ya mjadala inayoendelea kwenye mitandao kupitia tovuti ya Mchinga blog imechapisha kuwa mdudu kunguni anaweza kuishi takriban miezi 18 bila kufa na akaendelea kuwa hai.
Katika chapisho ambalo lina nukuu ya jumbe zifuatazo “Kunguni ni mdudu wa ajabu sana.Mdudu huyu hupenda kuishi maeneo waishipo binaadamu kwa kuwa chakula chake kikubwa ni damu y a binaadamu. Wadudu hawa hupenda kuishi vitandani na kujificha katika vipenyo vidogovidogo vya kitanda,au sehemu zinazofanana na hizo.
Kinachostaajabisha sana kwa mdudu huyu ni kwamba, KUNGUNI anaweza kukaa hadi miezi 18 bila kula na akiwa hai.katika hali hii kunguni huwa bapa zaidi na kubadilika rangi kutoka nyekundu/kahawia na kuwa Mweupe.Na punde tu baada ya kupata chakula(damu) Hubadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Je kuna ukweli wowote kuhusiana na chapisho ambalo limesambazwa kwenye mitandao?

- Tunachokijua
- Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kunguni mzima aliyelishwa vizuri na kuhifadhiwa katika joto la kawaida (zaidi ya 70°F ≈ 21°C) anaweza kuishi kati ya siku 99 hadi 300 katika maabara.
Inaelezwa kuwa kwa kawaida, mazingira ya makazi ya binadamu ni magumu zaidi kwa kunguni kuliko maabara (kupata chakula, mabadiliko ya joto na unyevunyevu, uwepo wa viuatilifu, kuepuka kupondwa, n.k.), na hali hizi hupunguza muda wao wa kuishi.
Utafiti wa hivi karibuni wa maabara umeonesha kuwa kukosa chakula kunaathiri sana uhai wa kunguni. Hii inapinga tafiti za zamani za Ulaya za miaka ya 1930 na 1940 zilizodai kuwa kunguni wanaweza kuishi zaidi ya mwaka mmoja bila kula. Ingawa hilo linaweza kuwa lilitokea kwa kunguni waliokuwa katika mazingira ya baridi kali sana (chini ya 40°F ≈ 4°C, hasa kutokana na ukosefu wa mifumo ya kupasha joto), kunguni wa kisasa waliokusanywa kutoka nyumba za Marekani hawaishi muda huo mrefu.
Kwa wastani, kunguni waliokosa chakula (katika hatua yoyote ya ukuaji) na kuhifadhiwa katika joto la kawaida hufa ndani ya siku 70. Inaaminika kuwa wengi wao hufa kutokana na kukosa maji mwilini (dehydration) badala ya njaa. Kwa kuwa kunguni hupata maji kupitia damu wanayonyonya pekee, ukosefu wa maji ndio tishio kubwa kwa uhai wao katika mazingira ya ndani ya nyumba.
Pia inaelezwa moja ya sababu zinazowafanya kunguni kujibana kwa wingi katika nyufa ndogo na mianya ni ili kudumisha mazingira madogo yenye joto na unyevunyevu unaofaa, jambo linalowawezesha kuongeza muda wao wa kuishi wanapokosa chakula.
Kunguni wachanga kabisa (hatua ya kwanza ya ukuaji – first instar) ndio walio katika hatari kubwa zaidi ya kufa wanapokosa chakula, kwani huishi kwa mwezi mmoja au chini ya hapo. Ingawa kunguni wa hatua ya pili (second instar) huishi muda mrefu zaidi (takribani miezi 1.0 hadi 2.5) kuliko wa hatua ya kwanza, bado muda wao wa kuishi bila chakula ni mfupi ikilinganishwa na wale wa hatua za juu zaidi au waliukua (ambao wanaweza kuishi hadi miezi 4 kulingana na aina).
Kunguni wa hatua ya tano (fifth instar) na wale waliokomaa ndio wanaovumilia zaidi kukosa chakula, lakini hata hivyo hakuna aliyedumu zaidi ya siku 135. Matokeo haya yanashangaza kwa sababu vyanzo vingi maarufu hudai kuwa kunguni watu wazima wanaweza kuishi zaidi ya mwaka mmoja bila kula.
Tofauti kubwa pia zilionekana katika muda wa kuishi bila chakula kati ya aina mbalimbali za kunguni (strains). Tofauti kubwa zaidi ilibainika kati ya wale waliokuwa na usugu dhidi ya viuatilifu (insecticide-resistant) na wale wasiokuwa na usugu.
Kunguni wenye usugu wa viuatilifu walionekana kuwa dhaifu zaidi wanapokosa chakula na walikufa haraka zaidi kuliko wale wasiokuwa na usugu.
Kwa ujumla, katika kila hatua ya ukuaji (iwe ni changa au aliyekomaa), kunguni wenye usugu waliishi nusu au hata theluthi moja tu ya muda ambao kunguni wasiokuwa na usugu waliweza kuishi bila chakula.