Dhahabu ni adimu lakini inapatikana sehemu nyingi, si Morogoro au TZ tu, bali duniani kote. Hata kwenye eneo la nyumbani kwako, ukikusanya udongo wa kutosha na kuuchenjua, unaweza kupata dhahabu kiasi.
Changamoto kubwa ni mbili. Kwanza, je, hiyo dhahabu unayoipata ina faida kiuchumi (economically viable)? Pili, je, uchimbaji wake ni endelevu au utachimba siku moja tu ukaimaliza na kuondoka?
Wakati mwingine kuna maeneo ambayo migodi mikubwa iliyaacha kwa sababu kwa makadirio yao yalikuwa yamefikia mwisho wa maisha ya mgodi (end of mine life). Akienda mchimbaji mdogo, eneo hilo linaweza bado kuwa na faida. Ukijibu hayo maswali mawili, utakuwa umepata picha halisi.
Pia, ni muhimu kuhakikisha eneo unalotaka kuchimba lina leseni halali ya shughuli za madini. Huwezi kufanya uchimbaji kwenye maeneo yaliyotengwa kwa matumizi mengine. Wamatumbi wanapaswa kujifunza kufuata sheria na taratibu za sekta ya madini.